DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
*****************************************************
#Post#: 1348--------------------------------------------------
Mabinti wanafunzi acheni kuwatega wavulana na wanaume
DIR By: Trainer
Date: February 8, 2015, 7:33 am
---------------------------------------------------------
Leo wapendwa wanafunzi ningependa kuwashauri watoto wa kike
yaani mabinti wasichana.
Mara nyingi mmekuwa mkitetewa na kulindwa sana na vyombo
mbalimbali vya kijamii. Lakini mnajua kuwa na nyie mnatakiwa
kujisitiri vizuri ili msiwatege wanaume na hatimae waanze
kuwasumbua kimapenzi.
Mtoto wa kike anashonewa sketi ndefu na wazazi wake lakini
akifika shuleni kama ni boding anapeleka ile sketi kwa fundi ili
apunguze urefu au anaikunja kwa nyuma ili mapaja yaonekane
vizuri upande wa nyuma . Sasa hapa unakuwa unategemea nini
kitafuata?
Kuwapa sketi ndefu ni kuwasaidia nyie msisumbuliwe na wanaume.
Ni kweli kuna wanaume ambao wenyewe wakiona sketi ya mwanafunzi
wanawaza kumtongoza mwanafunzi huyo, ila na nyie wasichana basi
mjitahidi kutowashawishi wavulana ili wawatongoze.
Tunajua mnaweka mitego hiyo ili wavulana au wanaume wawatongoze
ili muanze kupata pesa za matumizi na chipsi kuku lakini mjue
mwisho wake unaweza kuwa si mzuri. Utapewa mimba taaluma
itashuka na unaweza usifikie ndoto zako za kimaendeleo.
Kwa walionielewa nawashukuru wasionielewa wataelewa wakishapewa
mimba na kutelekezwa.
Una mchango wowote wewe mwanafunzi au mlezi au mzazi tujadili
hapa Asante.
*****************************************************
Page 1 of 1