DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
*****************************************************
#Post#: 1296--------------------------------------------------
Mambo 5 yatakayokusaidia kufaulu mtihani wako
DIR By: Trainer
Date: February 3, 2015, 1:34 pm
---------------------------------------------------------
Mwanafunzi jifunze mambo 5 yatakayokusaidia kufaulu mitihani
yako hapo shuleni unaposoma hata kama hakuna walimu wa kutosha
au vitendea kazi vya kutosha
Nitakupa siri ya kwanini wanafunzi wanaosoma shule za seminary
huwa wanafaulu vizuri zaidi ukilinganisha na shule zisizo za
seminary au shule zisizo za international.
Hakuna kitu cha pekee kilichopo huko saint somebody ambacho
kinawafanya wanafunzi hao wafaulu vizuri kwa wastai mzuri wa
darasa zima.
Siri ndiyo hii Yajue mambo matano yatakayokufanya ufaulu mtihani
wako hata kama upo kwenye mazingira magumu za kujisomea.
1.
HTML http://www.chatguest.com
Heshima na Nidhamu. Waheshimu walimu
wako hii itakufanya uwe rafiki wa walimu hao hivyo kutokana na
urafiki huo walimu hawatapenda rafiki yako afeli hata siku moja.
Heshima kwa wanafunzi wenzio. Usijikweze na kujiona labda wewe
ndiye unayejua sana hapo shuleni au wewe ndiye mwenye pesa
nyingi kati ya wanafunzi wote. Ukiwaheshimu wanafunzi wenzio nao
watakuona wa maana na hawatakutenga kwa chochote
kitakachokusaidia kufaulu mitihani yako.
Nidhamu kwa ujumla kufuata ratiba kama ilivyoandaliwa na shule.
Siku ya kuripoti tarehe 10 mwezi wa kwaza 2015 saa kumi kamili
kweli muda huo uwe shuleni umeshafika acha misemo ya Aaa mimi
nitavuta wiki mbili kwasababu wiki ya kwanza yote na ya pili
walimu hawataanza kuingia madarasani. Elimu sio ile ya kwenye
makaratasi tu kama unavyofikiri, Stadi za kazi nazo ni muhimu
kama wiki ya kwanza umezoea huwa mnafanya usafi wa mazingira
basi hakikisha na wewe unashiriki kikamilifu. Hii itakusaidia
kuondo hofu ya kuchelewa kuripoti na kupewa azabu zisizo za
lazima Pia unajifunza kuja kujitegemea baadae hata usipofanikiwa
kuajiriwa kwenye kazi zinazotaka cheti kina alama gani badala ya
mwajiriwa anauwezo gani.
2.
HTML http://www.chatguest.com
Saidia wenzio kitaaluma hata katika
mahitaji mengine ambayo unaona mtu fulani anauhitaji na wewe
unaweza kumsaidia. Wengi wanakuwa wachoyo wa kuwasaidia wengine
kitaaluma. Kama unajua hesabu za log vizuri na unatambua mtu
fulani haziwezi kabisa hesabu hizo basi mwite mwambie fulani
nataka leo nikufundishe hesabu za log mpaka uzielewe ni rahisi
sana. Sasa utashangaa faida utakayoipata kwanza ukimfundisha
mwezio wewe ndiyo ule ujuzi unakukaa zaidi ukiwa kwenye mtihani
utakumbuka siku ile uvyokuwa unamfundisha maria tabu mpaka
akaelewa kwahiyo utakuta unapata alama nzuri zaidi kwenye
mtihani wako.
Faida nyingine utapata vitini vya masomo mengine na past paper
ambazo hujawahi kuziona wala kuwa nazo hii ni kutokana na tabia
ya watu ambao wanakuwa na shida ya kuelewa masomo fulani huwa
wanatafuta material kwa hali na mali hivyo watu kama hao
ukioneshania ya kuwasaidia watakuona wa mana na kushare pamoja
nawe material walionayo. Hutahangaika kununua vitabu au vitini
vyote utavipata kwa marafiki kama una moyo mzuri wa kuwasaidia.
Lasivyo hawa watu watafungia vitini kwenye matranka yao na
hatimaye wote hamfaulu kwa kiwango kikubwa kama shule za saint
somebody
3. Jiwekee malengo ya kufaulu; Hata kama unaona wastani wa test
unazofanya haulizishi wewe weka malengo kuwa kama imetoka
umefeli basi uwe umefeli kwa alama B
HTML http://www.chatguest.com
ukiweka mengo hayo basi ikitokea
umefeli utafeli kwa alama C ambayo ni credit na itakuwezesha
kunedelea na ngazi za juu kama wengine wenye alama A.Usikate
taamaa hata kidogo, Unaweza kuta maajabu somo unaloliogopa sana
ndilo litakalokutoa.
4. Acha ulimbukeni. Ushalobalo, Usista du, Mapenzi shuleni hivyo
vyote utavifanya ukisha maliza masomo yako. Kwanza ukishamaliza
masomo. Ukianza vitu hivyo shueni taaluma itashuka tu.
5. Fanya mazoezi mara nyingi uwezavyo hapa sizungumzii mpira au
mazoezi ya kukimbia hapana nazungumzia kurudia rudia zoezi la
somo fulani. Mfano kama umejifunza definition ya what is biology
basi andika na kuikariri defintion hiyo hata mara miamoja.
Nimemkumbuka mwalimu moja mhindi alikuwa akisahihisha somo lake
akakuta umekosea neno moja tu kwenye sentensensi hiyo anakuagiza
uandika sentensi hiyo mara elfu moja kisha umpelekee asahihishe
tena sasa mwenzangu karatasi za kuandika hiyo sentensi mara elfu
moja gharama yake si umeshapunguza pesa za kununulia andazi la
kutafunia na uji uliowekwa chumvi ha ha ha ha Ila alikuwa
anasaidia sababu ukirudia rudia kitu huwezi kukisahau. Wazungu
wanasema "Practice makes perfect"
Naomba kwa leo tuishie hapa kama kuna typing error
HTML http://www.chatguest.com
popote hapo juu basi uniwie radhi hii
nikutakana na muda mfupi niliopata sikuweza kusahihisha
maandishi hayo.
Safari ijayo nitakupa mambo muhimu 5 ya kufuata ukiwa kwenye
chumba cha mtihani hata kama hukujiandaa vizuri kwa mtihani huo
bado utafaulu tu, na usipofuata mambo hayo hata kama ulijiandaa
vizuri bado utafeli tu au hutafaulu kwa kiwango kikubwa
Kama uandhani makala hii inaumuhimu kwa mwanafuzi basi like na
share huko facebook twitter na kwingineko
Una swali, shukani au nyongeza bonyeza "repy" hapo juu kulia.
*****************************************************
Page 1 of 1