DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 1218--------------------------------------------------
SHULE DAR HAINA VYUMBA VYA MADARASA, WATOTO WASOMEA CHINI YA
MITI
DIR By: udaku
Date: January 26, 2015, 8:40 am
---------------------------------------------------------
"SHULE DAR HAINA VYUMBA VYA MADARASA, WATOTO WASOMEA CHINI YA
MITI-MVUA KWAO LIKIZO
HTML http://1.bp.blogspot.com/-9h2rTxMMpbI/VMZCFAczMtI/AAAAAAAAaUQ/IT8ZdJj2uTg/s1600/SAKU%2B2.jpg
HTML http://3.bp.blogspot.com/-YHqAQKz1W9k/VMZCFStzrII/AAAAAAAAaUU/6hosXbRBBS8/s1600/SAKU.jpg
HTML http://4.bp.blogspot.com/-hbkh5rkXCLw/VMZCH4KMR0I/AAAAAAAAaUg/kME_agt8xRE/s1600/SAKU%2B1.jpg
HTML http://2.bp.blogspot.com/-2ueu582pFUs/VMZCJeIpo0I/AAAAAAAAaUo/UXRcGSZLWAM/s1600/SAKU%2B4.jpg
URITHI wa mtoto ni elimu, hiyo ni kauli mbiu ya shuleya Msingi
Saku iliyopo manispaa ya Temeke, Dar esSalaam lakini mazingira
ya usomaji shuleni hapoyanaweza yasitoae urithi huo kwa mtoto.
Wanafunzi zaidi ya 2500 wa shule hiyo wanasomakatika mazingira
magumu jambo linatia hofu kupataelimu bora ya watoto.Habarileo,
lilifika jana shuleni hapo na kupokelewa na walimu
waliochini ya miti hatua chache kutokamakundi mengine ya watoto
walio kaa mchangani chiniya Mwembe na miti ya
Mwarobaini.Ilikufanya kazi zake kikamilifu, ilifika
ofisi ya MwalimuMkuu, wa shule hiyo ambaye baada ya salamu
na waandishi kujitambulisha, mwalimu huyo aligomakutaja jina
lake na kuwafukuza waandihsi hao wahabari kwakuwa hawana barua
ya utambulisho kutokakwa Mkurugenzi.“Mimi nafanya kazi na
Mkurugenzi, mlete barua yautambulisho kutoka kwake vinginevyo
hamkupaswahata kukanyaga katika ardhi hii na muondoke
haraka,”alisema Mwalimu huyo Mkuu ambaye alitambulika kwa jina
la Salome Munisi.
Aidha Habarileo ilishuhudia wengi wakiwa nje wakicheza huku
wengine wakiwa wameketi chini yamiti kwa vikundi vikundi
wakitazama katika ubao na walimu wakifundisha. Walimu ambao
idadi yao inakadiriwa kuwa 30 wa shulehiyo wakiwa katika
ofisi yao chini ya miti wakiendeleana kazi ya kusahihisha
mitihani na kupitia madaftariya wanafunzi ambayo mengi yalikuwa
yamewekwachini. Katika vyumba saba vilivyopo vya madarasa
wanafunzi walionekana kujaa hadi mlangoni wakiwa wameketichini
huku madawati nayo yakionekana machache.Licha ya wingi huo wa
wanafunzi lakini baadhi yamashimo ya Choo klatika shule hiyo
yameonekanakutumika kama stoo ya kuhifadhia vitu.Mmoja wa
wawalimu ambaye hakutaka kutaja jina lakealisema shule hiyo ni
nzui wakati wa jua tu lakini Mvuaikinyesha ni kero kwani walimu
na wanafunzi wanakosamahali pa kukaa.
Pia wanafunzi wanaosomea chini ya miti mvuaikinyesha hawaji
shule maana watalowana na hata walimu pia hawata weza
kufundisha.“Hapa ni shida sana, tunafanya kazi katika
mazingiramagumu sana na huwezi amini kama upo Dar esSalaam, mvua
zikinyesha mfulululizo sisi ni likizo.Shule hiyo iliyo
inakabiliwa na uhaba wa vymba vyaMadarasa, madawati na vitu
vingine muhimu vyakufundishia na imefahamika kuwa darasa lililo
na watoto wachache ni 225 na mengine yanafika hadi
450.Baadhi ya walimu pia wamesema licha ya uhaba huo wamadarasa
lakini pia walimu 52 zaidi wanahitajika shulehapo huklu madawati
1,845 yakihitajika pamoja na vyumba vingine saba. Mapema Munisi
licha ya kukataa kuzungumza na waandishi wa habari, alisema kero
za shule hiyozinajulikana kila kona ya ofisi za
Mkurugenzi, AfisaElimu na wakaguzi wamekuwa wakifika
marakwa marakufanya ukaguzi."
Mi sijui bwana mtajua wenyewe
*****************************************************
Page 1 of 1