URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 1193--------------------------------------------------
       Ney wa Mitego na Jack Wolper Kuibua Mahusiano ya Kimapenzi Upya.
   DIR By: udaku
       Date: January 24, 2015, 2:02 am
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://3.bp.blogspot.com/-r2StwBm4E6w/VMM4eAO6QEI/AAAAAAAAnEA/WI4amBi2-Ew/s1600/Wolper%2B(1).jpg
       Na Musa Mateja
       BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia,
       hatimaye penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline
       Wolper na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
       limeibuka upya ambapo safari hii Nay ameamua kufunguka
       hadharani.
       Kwa mujibu wa chanzo makini,  wawili hao walianzisha uhusiano
       wao mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi
       kufikia hatua ya Nay wa Mitego  kuanika hisia zake mtandaoni.
       “Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba
       wake Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema
       chanzo chetu.
       Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego  kwenye
       mtandao wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya
       wapendanao kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
       Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo
       muda mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia  kisha
       Nay akaifuta posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.
       lipoulizwa Wolper kama kwa sasa ameamua kutulia na Nay wa Mitego
       na mipango ya uhusiano wao ipoje,  alikataa kufunguka moja kwa
       moja.“Kiukweli Nay ni mshikaji wangu tu, unajua nini? Kwa sasa
       siko tayari tena kumwanika bwana au mchumba wangu kama
       nilivyofanya mwanzo kwa Dallas, nitakuja kumweka wazi labda
       mwanaume nitakayezaa naye au atakayenioa kabisa,” alisema
       Wolper.
       Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper
       na hatua ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa
       ana mchumba mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:
       “Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini,
       mimi nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia
       peji yangu kama nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani
       hewani nikaamua kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu
       wa karibu na siogopi kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
       GPL
       *****************************************************
       Page 1 of 1