DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 1187--------------------------------------------------
TEKNOLOJIA YA INTANETI NI MKOMBOZI WA UMASIKINI TANZANIA
DIR By: HonestyQper
Date: January 23, 2015, 8:07 am
---------------------------------------------------------
“Mgeni njoo mwenyeji apone” ni msemo wa Kiswahili ulio na maana
iliyopo wazi kabisa,lakini wengi wao wameshindwa kuupatia maana
halisi. Je unataka kufahamu kiundani msemo huu una maana gani na
unakutoaje kwenye dimbwi la umaskini? Soma makala hii ya
kusisimua mpaka mwisho.
Teknolojia ya internet imekuja kwa kasi sana miaka ya hivi
karibuni barani Afrika, na katika nchi ambazo zimevamiwa na
teknologia hii ni Tanzania. Kama ijulikanavyo teknolojia ya
internet imerahisisha mambo kama mawasiliano na kuhifadhi
nyaraka kwenye program kama za google drive n.k
Teknolojia ya internet imekuwa kama msemo wa Kiswahili
usemao “Njoo mwenyeji mgeni apone” kutokana na kuwawezesha watu
wachache walio na uwezo wa kutumia teknologia hii kuweza
kuchagua fani wazipendazo na kuzisomea online. Mfumo huu umeweza
kuwasaidia watu wengi walio na kipato cha chini na cha kati
zaidi kutokana na kutumia gharama nafuu na kupata elimu iliyo na
ubora zaidi kulinganisha na elimu ya nchini, elimu hiyo mtu
anaweza kuitumia na kujitoa kwenye dimbwi la umasikini .
Teknolojia ya internet vile vile imewasaidia
wafanyabiashara mwenye kipato cha chini kuweza kutangaza
biashara zao kwenye mitandao ya kijamii kwa bei nafuu kabisa .
Kwa kuwa wao hawana uwezo wa kutangaza biashara zao kwenye Radio
na Televisheni, na badala yake gharama ambazo walikuwa watumie
wanazitumia kwenye maswala ya kujiendeleza wenyewe kibiashara.
Teknologia ya internet imeweza kutajirisha wachache kupitia
ajira za mtandaoni , watu wengi wamekuwa wakipata ajira
mtandaoni na kufanya kazi na kulipwa mamilioni ya shilingi
kutokana na teknologia ya internet. Mfano kuna mashirika kama
“Freelance” yanayotoa ajira zaidi ya milioni 1.6 mtandaoni au
mfano hapa Tanzania kuna mtandao unaoitwa “Chatguest” walionipa
kazi hii ya kuandika makala hii na kulipwa. Chatguest imetoa
vijana wengi kwenye dimbwi la umasikini kwasababu vijana wengi
wa kitanzania hawapendi kufanya kazi au kufikiria basi Chatguest
imeamua kuwaambia “haya basi chezeni game tuwalipe” Bado mwamko
ni mdogo pia. Mgeni amekuja Tanzania basi sisi wenyeji inatakiwa
tupone kwa kutumia fursa hii ya kipekee tuweze kushindana na
mataifa yaliyoendelea. Wewe kijana ambaye una uwezo wa kutumia
teknologia hii itumie kujiendeleza kielimu na kujiajiri kwenye
mitandao na kuikomboa jamii yako kwenye umasikini.
Kwenye makala yangu hii napenda kutoa mawazo yafuatayo ili
kuweza kufanikisha zaidi mambo niliyoyazungumzia hapo juu.
1.
kuhakikisha teknolojia ya internet inatumika kwenye maswala ya
faida zaidi ili kuikomboa jamii na umasikini.
2.
na vile vile makampuni yanayotoa huduma ya internet kupunguza
gharama ya matumizi ili kwezesha watanzania walio na kipato cha
chini waweze kufaidika na teknologia ya internet .
Mambo hayo yakifanyika msemo wa “Njoo mgeni mwenyeji apone”
utatutoa watanzania kwenye umasikini. Na anza sasa kutajirisha
jamii yako kwa kuipa makala hii ALAMA ya “NDIO” . Asanteni
#Post#: 2147--------------------------------------------------
Re: TEKNOLOJIA YA INTANETI NI MKOMBOZI WA UMASIKINI TANZANIA
DIR By: stakeholder
Date: August 13, 2015, 2:04 pm
---------------------------------------------------------
Makala imefungwa. Haijafikisha idadi ya kulipwa, mwandishi
unashauriwa kuandika nyingine ili ulipwe
*****************************************************
Page 1 of 1