DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
*****************************************************
#Post#: 1178--------------------------------------------------
Wema sepetu kumpeleka diamond platinum polisi
DIR By: udaku
Date: January 23, 2015, 5:40 am
---------------------------------------------------------
HTML http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/Diamond-na-Wema-nzuri_full1-300x191.jpg
MKALI wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu
‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye
ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa
kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya
Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay
akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa
makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume
makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu
wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai
kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia
dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi
Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali
ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo
ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la
kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa
makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya
mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha
hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati
wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa
kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki
kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora
angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya
mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia
ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote
angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,”
alisema.
Hata hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili
ya ziara yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la
polisi kwa barua ya wito kufika kituoni pindi atakaporejea
nchini, huku mama yake mzazi akifikishiwa ujumbe huo nyumbani
kwake.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho
kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha
wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa
jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika
ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe
muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama
wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na
utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti .
MTANZANIA ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae
alieleza hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba
apewe muda kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu
ya suala hilo, lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza
asubiriwe.
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu
Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa
hazina ukweli wowote mtanzania fikra yakinifu. Mwisho wa story.
Eti nauliza unaweza kumkoesha mpenzi wako pesa? Je atakulipa?
*****************************************************
Page 1 of 1