DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 1177--------------------------------------------------
AJUZA WA MIAKA 90 ANASOMA DARASA LA NNE Kweli elimu haina mwisho
DIR By: udaku
Date: January 23, 2015, 5:30 am
---------------------------------------------------------
HAYA SI MAAJABU? AJUZA WA MIAKA 90 ANASOMA DARASA LA NNE
HTML http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/01/23/150123014307_gogo_512x288_bbc_nocredit.jpg
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria
masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye
mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani. Akiwa
ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na
amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza
mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya
wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake. Prissilla alijiunga
na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka mitano
iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake
cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka
sitini na mitano iliyopita. Darasani Priscilla anawasaidia
wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14
na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo
urithi wao. Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi
katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa
na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma
pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo. Lugha ambayo Priscilla
anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin
kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua
kujiunga na shule katika umri wake. Sababu kubwa ambayo amekuwa
akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa
umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani
anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana
watoto. Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto
ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini
hawako shuleni. Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi
shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa
sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza
muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila
msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende
shuleni.
Chazo BBC
*****************************************************
Page 1 of 1