URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Sports and entertainments 
       *****************************************************
       #Post#: 1152--------------------------------------------------
       Hapatoshi leo England, Man City vs Arsenal
   DIR By: mastory
       Date: January 18, 2015, 12:47 am
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://3.bp.blogspot.com/-Yjb2duwyWi8/VLtQsEvyqeI/AAAAAAAAOXI/-YN9Rz3m_2E/s1600/EPL.jpg
       KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea leo kwa
       mechi mbili likiwamo linalovuta hisia za wengi litakalochezwa
       kwenye uwanja wa Etihad mjini Manchester kati ya wenyeji
       Manchester City dhidi ya Arsenal.
       Pambano jingine la leo litazikutanisha timu za West Ham Utd
       watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Hull City katika uwanja wa
       Boleyn.
       Mabingwa watetezi Manchester City wataikaribisha Arsenal
       wakitoka kulazimishwa sare katika mechi yao ya mwisho, ilihali
       Arsenal wakitoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya
       Stoke City.
       Ingawa Arsenal itakosa huduma za beki wake Mathieu Debuchy
       aliyeumia bega katika mechi yao iliyopita sambamba na kuwakosa
       wakali wengine ambao ni majeruhi kama ambavyo watetezi Man City
       watakavyokosa huduma za wakali wake akiwamo Yaya Toure na
       Wlifried Bony waliopo Afrika kwa sasa..
       City itakuwa ikisaka ushindi nyumbani kuweza kuendelea kuwabana
       Chelsea wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakati wao wakiwa wapo
       nafasi ya pili.
       Watetezi hao wana pointi 47 wakati wapinzani wao Arsenal wakiwa
       na pointi 36 wakishika nafasi ya tano.
       Ligi hiyo itaendelea kesho kwa pambano moja tu
       litakalozikutanisha timu za Everton dhidi ya West Bromwich
       Albion mechi itakayochezwa kwenye uwanja wa Goodson Park.
       credit  micharazomitupu blog
       *****************************************************
       Page 1 of 1