URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
       *****************************************************
       #Post#: 1150--------------------------------------------------
       Matokeo ya kidato cha pili 2014 haya hapa 
   DIR By: Nadia
       Date: January 17, 2015, 12:29 pm
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://2.bp.blogspot.com/-2kwVLmJzd_0/VLqhd09Rs-I/AAAAAAAATyI/Kz1vl6ZRljg/s1600/1.jpg
       Baraza la Mitihani la Taifa nchini Tanzania NECTA leo limetoa
       matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili mwaka 2014 kwa
       wanafunzi waliofanya mtihani huo unaowapa fursa ya kuendelea na
       kidato cha tatu.
       
       Akisoma taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari katika ofisi za
       NECTA jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles
       Msonde amesema kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2014 kimeongezeka
       kwa asilimia 3.32 kutoka asilimia 89.34 mwaka 2013 hadi asilimia
       92.66 mwaka 2014.
       
       Amesema waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 453,191 lakini
       waliofanya mtihani walikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40 na
       kwamba wanafunzi 47,987 sawa na asilimia 10.60 hawakufanya
       mtihani huo kwa sababu tofauti.
       
       Dkt Msonde amesema Jumla ya wanafunzi waliofaulu kwa kupata
       alama zinazowaruhusu kujiunga na kidato cha Tatu ni 375,434 sawa
       na asilimia 92.66 ambapo kati yao wasichana ni 195,328 na
       wavulana ni 180,106.
       
       Jumla ya wanafunzi 29,770 sawa na asilimia 7.34 wamefeli kwa
       kushindwa kufaulu kwa kiwango kinachotakiwa, na hivyo
       watalazimika kukariri darasa.
       
       Dkt Msonde amesema kuwa matokeo hayo yamepangwa kwa mfumo
       Wastani wa Pointi (GPA) ambapo madaraja yamepangwa kwa
       Distinction, Merit, Credit, Pass na Fail.
       Jumla ya wanafunzi 180,965 sawa na asilimia 44.66 wamefaulu kwa
       madaraja ya juu (Distinction, Merit na Credit).
       
       Ametaja ufaulu kwa kila daraja kuwa ni kama ifuatavyo
       Distinction wanafunzi 35,656 sawa na asilimia 8.8
       Merit wanafunzi 57,945 sawa na asilimia 14.30
       Credit wanafunzi 87,364 sawa na asilimia 21.56
       Pass wanafunzi 469 sawa na asilimia 47.99.
       
       Kwa upande wa ufaulu katika masomo, Dkt Msonde amesema kuwa somo
       lililoongoza kwa ufaulu ni History ambalo wamefaulu kwa asilimia
       90.71 na somo lenye ufaulu mdogo zaidi ni Basic Mathematics
       ambalo ufaulu wake ni asilimia 18.15.
       
       Masomo yenye ufaulu mzuri ni Civis, History, Kiswahili na
       English ambapo ufaulu ni asilimia 84 yakifuatiwa na Geography,
       Biology na Book-keeping yenye ufaulu wa kati ya asilimia 50-70
       na masomo yenye ufaulu wa chini ni Chemistry, Basic Maths,
       Physics, Commerce na Agriculture ambayo ufaulu wake ni chini ya
       asilimia 50.
       
       Amesema katika baadhi ya masomo, baadhi ya wanafunzi wameonesha
       umahiri kwa kufaulu kwa kupata alama 100%.
       
       Masomo hayo ni
       Englishi wanafunzi 41
       Basic Maths wanafunzi 9
       Biology mwanafunzi 1 na Book keeping mwanafunzi mmoja.
       
       Ameipongeza serikali kwa kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa
       Sasa (BRN) kwa madai kuwa ndiyo sababu ya matokeo haya kuwa
       mazuri lakini ametaka juhudi ziendelee kufanywa katika masomo
       yenye ufaulu wa chini.
       Bonyeza link kuangalia matokeo ya kidato cha pili 2014/20115
  HTML http://necta.go.tz/matokeo2015/
       #Post#: 1281--------------------------------------------------
       Re: Matokeo ya kidato cha pili 2014 haya hapa 
   DIR By: stakeholder
       Date: February 2, 2015, 11:18 am
       ---------------------------------------------------------
       Ukijiunga leo kwenye mtandao huu unaweza bahatika vocha za simu
       bure kupitia email yako. Kujiunga ni bure na ni dakika 2 tu
       bonyeza hapa
  HTML http://www.chatguest.com/index.php?action=register
       *****************************************************
       Page 1 of 1