URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
       *****************************************************
       #Post#: 1133--------------------------------------------------
       "TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU AWAMU YA 2 KWA
       MWAKA WA MASOMO 2015/2016
   DIR By: Hamis abdul
       Date: January 15, 2015, 1:05 pm
       ---------------------------------------------------------
       "TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU AWAMU YA PILI KWA MWAKA
       WA MASOMO 2015/2016
       TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU AWAMU YA PILI MWAKA WA
       MASOMO 2014/2015
       
       Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
       anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu yatakayoanza Januari 2015
       kama ifuatavyo:
       KUNDI LA I
       Waombaji wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu ambao
       waliwasilisha maombi yao Wizarani awamu ya pili kwa ajili ya
       kuchaguliwa kujiunga na mafunzo mwaka wa masomo 2014/15.
       Waombaji hawa wamechaguliwa na kupangiwa vyuo kulingana na
       Programu za mafunzo (Angalia orodha iliyoambatanishwa).
       Waliochaguliwa wanatakiwa kufanya maandalizi ya kujiunga na vyuo
       walivyopangiwa kwa kuzingatia maelekezo ya fomu zilizoambatishwa
       za kujiunga na chuo husika. Tarehe rasmi ya kuripoti vyuoni
       itatolewa mapema Januari 2015.
       
       KUNDI LA II
       Kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka wa
       masomo 2014/15 katika programu zifuatazo:
       1.     Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali na Stashahada ya
       Kawaida ya Elimu ya Msingi – Sayansi (Tarajali) (Miaka 3)
       Wanaotakiwa kuomba mafunzo haya ni:
       a)     Wahitimu wa kidato cha IV 2013 ambao hawakupata nafasi za
       kujiunga na kidato cha V katika shule za sekondari za Serikali
       mwaka wa masomo 2014/15. Orodha ya wahitimu husika imeambatishwa
       na tangazo hili (Angalia orodha iliyoambatanishwa).
       b)      Waombaji wengine wenye ufaulu usiopungua Daraja la III
       katika mtihani wa Kidato cha IV uliofanyika kwenye kikao kimoja
       (single sitting) kati ya mwaka 2004 na 2013.
       
       Mafunzo yatatolewa katika vyuo vifuatavyo:
       a)    Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali
       Ilonga, Mhonda, Mtwara (K), Mtwara (U), Sumbawanga, Kinampanda,
       Tarime, Katoke, Tandala, na Tabora.
       b)   Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi – Sayansi
       (Tarajali)
       Tukuyu, Kasulu, Songea, Korogwe, Butimba, Mpwapwa, Morogoro, na
       Kleruu.
       2.     Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi -Walimu kazini
       (Miaka 2)
       Wanaotakiwa kuomba mafunzo haya ni: Walimu Kazini shule za
       msingi (In-Service) ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ wenye uzoefu wa
       kazi usiopungua miaka 2 na  walio katika mpango wa mafunzo kwa
       mwaka wa masomo 2014/15 katika Halmashauri zao.
       
       Mafunzo yatatolewa katika vyuo vya Bustani na Marangu.
       
       Waombaji wenye sifa watume maombi yao kwa njia ya “Online” kwa
       kujaza fomu zinazopatikana kwenye Tovuti ya NACTE:
       www.nacte.go.tz au kujaza fomu ya maombi kwa  kupakua fomu ya
       maombi hapa, soma kwa umakini fomu hyo, ijaze na kutumwa kwa:
       Katibu Mtendaji
       Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi,
       S. L. P. 7109,
       Dar-es-Salaam,
       Tanzania.
       au ziletwe moja kwa moja katika ofisi zetu: Makao Makuu - Dar es
       salaam na ofisi za kanda zilizopo mikoani.
       Mwisho wa kutuma maombi ni terehe 31 Desemba 2014. Orodha za
       waombaji watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo haya na tarehe
       rasmi ya kuripoti vyuoni itatolewa mapema Januari 2015.
       
       
       Imetolewa na:
       KATIBU MTENDAJI
       BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
       DESEMBA 2014"
       Unaweza soma habari hiyo kwenye tovuti husika ya nacte
       *****************************************************
       Page 1 of 1