URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
       *****************************************************
       #Post#: 1017--------------------------------------------------
       Elimu ya Sekondari itakuwa BURE kuanzia 2016 - Jakaya Kikwete 
   DIR By: udaku
       Date: January 1, 2015, 12:16 am
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://2.bp.blogspot.com/-d_blVTw_Bmo/VKThEQXhIRI/AAAAAAAAl0U/VeYroLLkico/s1600/jk...jpg
       Katika Salaam za Mwaka Mpya Kutoka kwa Rais Jakaya kikwete
       Amegusia Swala la elimu na Kusema kuhusu Elimu ya Secondary
       Mwaka ujao itakuwa ni Bure.
       Nanukuu kama Ifuatavyo:
       'Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
       Ndugu wananchi;
       Mafanikio mengine tuliyopata mwaka huu ni kukamilika kwa Sera ya
       Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014. Hii ni hatua muhimu sana katika
       maendeleo ya elimu nchini hakuna badala yake. Sera mpya inalenga
       kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu
       zitakazowezesha Watanzania wengi zaidi kupata fursa za elimu
       iliyo bora na inayolinga na wakati tulionao. Jambo jipya sana na
       la kihistoria katika Sera mpya ya Elimu ni dhamira ya Serikali
       ya kuondoa ada katika elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016.
       Mpaka sasa hatuna ada kwenye shule za msingi, sasa wakati
       umefika kufanya hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kwa mujibu wa
       maelezo hayo ya Sera, nimekwishatoa maagizo kwa Wizara ya Elimu
       na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
       Mitaa, Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango kuanza kutafakari
       namna jambo hilo litakavyotekelezwa.' Jakaya Kikwete"
       Maoni yako kama mdau wa elimu hii inawezekana? Itakuwa bure
       kweli au michango kibao?
       *****************************************************
       Page 1 of 1