DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
*****************************************************
#Post#: 966--------------------------------------------------
FUMANIZI SIKU YA CRISMASS, AMA KWELI MCHEPUKO SIO DILI
DIR By: udaku
Date: December 29, 2014, 2:28 am
---------------------------------------------------------
HTML http://api.ning.com/files/kdMiOwfaxve9UDPHVqZC5YH1*UdtXoPC4caUphHmPyscuTiqnbg4WYfrrSzM4Tb7jz1ZRbvJ8E6Nzp-etK803-FwBcVq83cx/mchepu.jpg
[img]
HTML http://api.ning.com/files/kdMiOwfaxvcUvvjrspK6osxMnx8B0Adi1ctIj4kjcsxTTiBGxv8QNJIRjNJKCr9T8fLdjPHeTgvuGXyEJ83UCFRDJMivDrzL/IMG20141224WA0021.jpg?width=650[/img]
Shabaash! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mikocheni A, Dar, Catherine
Kayombo ‘Catty’ anadai kumfumania mumewe aliyemtaja kwa jina la
Excavery Kayombo akiwa na mchepuko alioutaja kwa jina la Mariamu
Kauke ‘Mamuu’ ndani ya Sikukuu ya Krismasi ‘X-Mas’, Ijumaa
Wikienda limesheheni.
Mchepuko unaojulikana kama Mariamu Kauke ‘Mamuu’ ukiwa katika
kitanda cha mume wa mtu.
MAJIRANI WAPENYEZA UBUYU
Tukio hilo la aina yake lilitokea majira ya mchana maeneo ya
Mikocheni A ambapo Catty anayedai kupigwa na mumewe na kwenda
kwao, alipata taarifa (ubuyu) kutoka kwa majirani kuwa mumewe
ameingiza mwanamke nyumbani kwake na wanajiachia na
kujimwayamwaya kila mahali ndani kama kumbikumbi.
Mchepuko ukikemea kupigwa picha dirishani.
Baada ya kupata taarifa hizo, Catty alikwenda nyumbani kwake
kisha akamfuatilia mumewe na mwanamke huyo hatua kwa hatua
kupitia dirisha la chumba chao ‘kwa baba na mama’.
Mume wa mtu, Excavery Kayombo akiwa na mchepuko huo.
FULL KUJIACHIA
Catty alidai kwamba alimshuhudia mwanamke huyo akiwa amejiachia
na kujimwayamwaya kwenye kitanda chake akiwa na kijitaulo huku
mumewe akiingia bafuni kuoga baada ya kufanya yao.
Alisema baada ya kujionea kila kitu laivu, Catty aliwafotoa
picha kadhaa kwa kutumia kilongalonga chake cha kiganjani ambapo
mchepuko huo ulimshtukia na kumuita mume wa Catty ambaye alikuwa
bafuni akimwambia kuwa mkewe amefika huku akiwa hana wasiwasi.
Mke halali wa Bw. Excavery Kayombo, Catherine Kayombo ‘Catty’.
BILA WASIWASI
Catty alidai kwamba mwanaume huyo alitoka bafuni bila kujali
picha alizokuwa akipigwa na mkewe kupitia dirishani na kumwambia
kuwa hata akipiga na kuzipeleka magazetini yeye hajali hata
kidogo. Akafunguka kuwa ameamua kuishi na Mamuu na atamuoa
‘soon’.
Mchepuko ulionaswa, Mariamu Kauke ‘Mamuu’.
Kama hiyo haitoshi, Ijumaa Wikienda lilipofika eneo la tukio
lilishuhudia mambo ambapo Catty ambaye amezaa na mumewe huyo
watoto wanne, aliwaambia waandishi wetu kuwa anachotaka kwa sasa
kwa mwanaume huyo ni talaka tu.
Paparazi akipata undani wa habari kutoka kwa Catherine Kayombo
‘Catty’(mke wa Bw. Excavery Kayombo) .
Katika hali ya kushangaza, mumewe huyo alimwacha Catty nyumbani
hapo na kuondoka na mchepuko wake kila mmoja akiwa na gari lake.
Mume alikuwa na gari lake aina ya Toyota Prado na mwanamke
alikuwa na gari lake aina ya Toyota Mazda.
Gari la Bw. Excavery Kayombo likiwa eneo la tukio.
WAKUTANA BAA
Baada ya Catty kuondoka nyumbani hapo akiwa na majirani zake,
walikwenda kwenye baa moja iliyopo jirani na nyumbani kwake
iitwayo Five Ways ambapo walimkuta tena mumewe huyo akiwa na
mchepuko wake wakinywa moja moto, moja baridi bila wasiwasi
wowote.
Waandishi wetu walipofika eneo la tukio walimshuhudia mwanaume
huyo akikimbilia kwenye gari lake huku mchepuko wake ukiwa
kwenye gari la nyuma wote wakiondoka ambapo taarifa za
kiintelijensia zilidai kuwa walikuwa wakirudi tena nyumbani
kwake.
Gari la mchepuko likiwa eneo la tukio.
BOFYA HAPA KUMSIKIA MWENYE MUME
“Yaani hamuwezi kuamini huyo mwanaume alivyonifanyia! Eti
ananijibu bila aibu kwamba atamuoa huyo mwanamke wake. Mimi sina
tatizo nimeomba talaka yangu anipatie nijue ustaarabu wangu
maana tabia yake hii imenichosha, nimemvumilia sana,” alisema
Catty akiwa ‘amepaniki’.
Bw. Excavery Kayombo akiwa na mchepuko wake Kwenye baa.
Alipotafutwa mwanamke anayetembea na mume wa Catty, Mamuu
alisema: “Nilipofika ndani ya nyumba sikumwona mwanamke yeyote.
Ninavyojua watu hawa wameachana ndiyo maana nimeamua kukaa hapa,
mimi siyo mtu nisiyekuwa na akili najitambua.”
Kwa upande wake mwanaume huyo hakutaka kuzungumza na wanahabari
wetu zaidi ya kukimbilia kwenye gari na kujifungia.
Chanzo:tuangazeblog
*****************************************************
Page 1 of 1