URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 847--------------------------------------------------
       DARASA LA MAPENZI:Wanaume mnajua hili: Mfanyie mwanamke
       akuzidishie raha 
   DIR By: udaku
       Date: November 2, 2014, 2:08 am
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://3.bp.blogspot.com/-Wq6AFc9ovV8/VEO3T5n39FI/AAAAAAAABHs/3E42mmpnCz8/s640/black-love.jpg
       MAMBO vipi ndugu zangu? Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena
       kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa safu yetu hii. Tumshukuru
       Muumba wetu kwa kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi ya
       hapo tumshukuru pia kwa kutuumbia kitu mapenzi au siyo jamani?
       Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli
       usiopingika kwamba mapenzi ndiyo maisha yetu.
       Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko,
       lakini mwisho wa siku tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha
       na kufurahia maisha na wapenzi wetu.
       Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu na amani
       katika maisha ya kimapenzi na wapenzi wetu, waume zetu au wake
       zetu katika siku zote za maisha yetu.
       Ndugu zangu, Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani
       katika maisha yetu.
       Kwa maana hiyo, wale wanaoyachezea na kuyavuruga mapenzi kwa
       makusudi kwa kuumiza hisia za wenzao kisha kuwasababishia vilio
       si watu wa kupendeza mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini
       maana ya mapenzi.
       Wanawake ni watu wa kuheshimika na kupewa furaha wanayohitaji.
       Unapompata mwanamke anayekupenda na kukuheshimu, huna sababu ya
       kumfanya ajute kuwa na wewe.
       MPENDE NA MTHAMINI!
       Yawapasa wanaume mfahamu kuwa, wanawake ni zawadi kwenu, pumziko
       na tulizo la mioyo yenu. Wanawake ndiyo raha na amani kubwa ya
       maisha yenu.
       Kosa kubwa mnalofanya wanaume ni kuutumia vibaya mfumo dume hasa
       katika suala nyeti kama mapenzi.  Mapenzi si ubabe, mapenzi ni
       upole na ukarimu.
       Pamoja na kwamba mmebarikiwa kwa kupewa nafasi ya kuwa kichwa
       katika nyumba lakini linapokuja suala la kurekebisha tofauti
       zinazojitokeza katika uhusiano wenu, si vyema kutumia njia za
       kibabe.
       Niwaambie kitu, wanawake ni wa hisia zaidi na waliobarikiwa kuwa
       na upendo wa hali ya juu na ndiyo maana wakapewa dhamana ya
       kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na pia kumnyonyesha na
       kumlea kwa miaka kadhaa, wewe mwanaume ungeweza?
       Nasema ni watu wa hisia kwa sababu, hivi uliwahi kufikiri ni kwa
       nini wanawake huridhika na kujisikia poa kweli wanapopewa zawadi
       kama ya maua na kadi zenye ujumbe wa mapenzi ukilinganisha na
       wanaume?
       Unafikiri ni kwa nini wana machozi ya haraka wanapotendwa? Au
       unafikiri ni kwa nini wanapenda kutumiwa ‘love sms’ zaidi kuliko
       kupigiwa simu? Jiulize.
       Mimi nawaona wanawake kama watu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa
       dhati.  Mkumbuke wanawake ndiyo mama zetu, walezi wetu na ndiyo
       nyumba zetu. Jaribuni pia kujicontroo na huo mnaouita ukijogoo
       kwamba eti ninyi ni watu msioridhika na mpenzi mmoja.
       Jaribuni kufanya kila mnaloweza kuifuta ile dhana ya kwamba
       wanaume hawaaminiki hata kidogo. Ridhika na mpenzi uliyenaye,
       heshimu hisia zake na thamini mapenzi yake kwako na mpe ile kitu
       roho inapenda!
       Ni hayo tu kwa leo
       credit
  HTML http://tuangaze.blogspot.com/
       *****************************************************
       Page 1 of 1