DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
*****************************************************
#Post#: 795--------------------------------------------------
AIBUUU:: NI SHIDA MKE, MUME WAVUANA NGUO LIVE WAKIZICHAPA
HADHARANI
DIR By: udaku
Date: October 3, 2014, 12:32 am
---------------------------------------------------------
HTML http://1.bp.blogspot.com/-vI5fF4K7fSo/VC4f4RvT4II/AAAAAAAAqfs/5LGhueM6UxY/s1600/AIBUUU3.jpg
Hii ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno
na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga
jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na
kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea
‘sinema’ ya bure.Timbwili zito likianza kati ya njemba mmoja
anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata. Tukio
hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa
Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo
kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa
kupata kilaji.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi
nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini
ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi,
pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake
huyo.
[img]
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtyko1Z-BbXPfos5WncL-a0IBCOnCwh6tm6Ul6yrkp8e5PIoGWSkvOGdh9nDBJXpzGJ-sc3P49hRfv2ABcgsbm9F/IMG_3351.jpg?width=650[/img]
Mke akimlia 'taimingi' kumbwaga mume wake kwa mweleka.
MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo
wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi
akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye
alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtxgpqHZBxCPxUcCA41Br4ic3XS8UCLTuvOxjZ1ymBUnqiwLhDbTzX4Fw7XnB2L0Iq6knI4DbGb9aHtWrnixQI-r/IMG_3352.jpg
Mara Puuuuu...!! wote chini “Sasa akiwa pale baa, alizidi
kunogewa na masaa yalizidi kupotea ndipo Zeno alirudi nyumbani
na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo huku akisikia harufu
kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua
na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka
mkewe,” kilidai chanzo hicho.
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtzCM9NlntyfYtVWDNvNLvnlKh0zNLqeildfPtMsnWmNq6potFROZ-*KhcYH4rQFQT5kD4q7uQhXr8Ljt88B2Hav/IMG_3364.jpg
Mume (Bw Zeno) akimburuta mkewe kwa ghadhabu. AMUIBUKIA BAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika
sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia
‘kunyonya’ kilevi kikali. ZACHAPWA
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa
makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe
na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa
katika hali ya kuzidiwa na kilaji.
[img]
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtzW*YMXu4rI6Rz7KNHbg5EIu24BIu7*X548wQHR0iZ-yKNsyE5*grDAwf6Vy-rpgnHbv9BfjyHSGTHpfDhDm5J9/IMG_3343.jpg?width=650[/img]
Wote wakichukua uamuzi wa kuzima timbwili hilo. LAHAMIA NJE YA
BAA
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili
wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa
walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa
mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini
walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtwt6Ry9ZrLzQZt6InWy1g24SEmNaEX-lJX2VtYU3rw7x8ajUEwaaa64S1wbt6ZOA7muZx30PPpJFI3Hk8eQYixi/IMG_3334.jpg
Mke(Bi Mwajuma Mtata) akijaribu kuzuia kupigwa picha na kamera
za wanahabari. WARUDI NYUMBANI
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na
kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi
nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza
kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
HTML http://api.ning.com/files/45z4r7ugTtxV6pJz4xQ3KfkIvlRsMJLWKkkvInmgJOSQkXnH5ioFj5*Rll2hJa8rzgk2fE-hBnIEZTqypA95aFNt3BClXkW6/IMG_3341.jpg
Jirani akihoji kulikoni mpaka iwe hivi... ETI WAMEYAMALIZA!
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda
mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari
wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana
msamaha.
Chanzo GPL
#Post#: 841--------------------------------------------------
Re: AIBUUU:: NI SHIDA MKE, MUME WAVUANA NGUO LIVE WAKIZICHAPA
HADHARANI
DIR By: Nsolo
Date: October 18, 2014, 4:00 am
---------------------------------------------------------
Yameisha kwa uchafu wa sifa.
*****************************************************
Page 1 of 1