URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 787--------------------------------------------------
       DUH NDOA NDOANO FUNDI AJINYONGA KISA MGOGORO WA KIMAPENZI SOMA
       ILIVYOKUWA HAPA
   DIR By: udaku
       Date: September 30, 2014, 4:59 am
       ---------------------------------------------------------
       KATIKA hali ya kushangaza, mtu mmoja ambaye ni fundi seremala
       aitwaye Emmanuel Carlos, mkazi wa Kwabinyau Magomeni jijini Dar
       amekutwa akiwa amejinyonga saa mbili asubuhi Septemba 23, mwaka
       huu katika kile kinachodaiwa kuchoshwa na mgogoro wa kifamilia
  HTML http://1.bp.blogspot.com/-JBHXoOuwi4w/VCovYdDFGSI/AAAAAAAAp-8/-1nn0nIsMxk/s1600/kufa.jpg
       Emmanuel Carlos enzi za uhai wake.
       Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, kwa muda mrefu,
       marehemu alikuwa na mgogoro usioisha na mkewe Mariamu Suleimani
       uliosababisha wawili hao kulala katika vyumba tofauti ndani ya
       nyumba yao.
       Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kutokana na ugomvi huo,
       marehemu alikuwa akirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na
       kumtukana matusi mkewe hukubaadhi wakienda mbali na kudai
       alikuwa haachi hela ya matumizi.
       Hata hivyo, mkewe marehemu anadaiwa kuwa na biashara yake ya
       samaki na alikuwa akijituma ili kuhakikisha anapata nauli ili
       arejee nyumbani kwao.
       Kwa mujibu wa maelezo yaliyopatikana, mtu wa kwanza kujua kuhusu
       suala hilo alikuwa ni kijana wake mwenye umri wa miaka saba,
       Celestine Carlos aliyekwenda chumbani kwa baba yake kuomba hela
       ya shule, ambapo alimkuta akining’inia kwenye dari baada ya kuwa
       amejifunga kamba kwenye feni.
       Akizungumza na waandishi wetu Mariamu alisema kuwa siku moja
       kabla ya tukio, mumewe alirudi nyumbani na kumtukana huku akilia
       na kumwambia kuwa atamkumbuka sana katika maisha yake na kwamba
       kabla ya kupambazuka mmoja wao atakuwa amekufa.
       “Siku iliyofuata alipoamka alinikuta naosha vyombo, akanitazama
       kwa jicho baya kisha akaenda chumbani kwake ambako alijifungia.
       Nusu saa baadaye alikuja mwanaye Celestine na kuniomba hela ya
       shule, nikamwambia aende akachukue kwa baba yake, alipoingia
       akarudi na kuniambia baba yake ananing’inia, jambo nililoona
       kama utani lakini baadaye nilienda na kumkuta akiwa
       amejinyonga,” alisema Mariamu huku akilia kwa uchungu.
       Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Jumanne Mneka alikiri
       kufahamu mgogoro wa familia hiyo na kusema walikuwa
       wakiwasuluhisha kila mara.
       *****************************************************
       Page 1 of 1