URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 718--------------------------------------------------
       JINSI MWANAMKE ANAVOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME
   DIR By: udaku
       Date: September 20, 2014, 11:30 pm
       ---------------------------------------------------------
  HTML http://1.bp.blogspot.com/-1r_aYuIv4Z0/VBxiCQ0-heI/AAAAAAAAAjM/v30ws2V4Ofs/s640/musevenis-daughter.jpg
       1: KAULI
       Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka
       kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA.
       Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa
       hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia
       ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.
       Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu
       kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na
       kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu
       wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku
       hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
       2 : UJUZI
       Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye
       tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si
       wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki
       tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo
       anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile
       hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
       Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni
       watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume
       ajione kama mgeni wa mchezo huo.
       Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini
       pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na
       kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia
       tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
       Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa
       masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango
       kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi,
       asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya
       juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha
       wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
       3:USAFI
       Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume
       matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu
       wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni
       wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze
       msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili
       ni muhimu sana katika mapenzi.
       4:GUBU
       Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa
       nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi
       yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi,
       usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha
       tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
       Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi
       huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo.
       Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii,
       huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake
       wa nje kuliko wake zao hao.
       5:USALITI
       Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume
       kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona,
       kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu
       ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo
       humuondolea hamu ya tendo
       Source bekamtanzania
       *****************************************************
       Page 1 of 1