URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Makala Bora
       *****************************************************
       #Post#: 3307--------------------------------------------------
       MAKALA:MBINU ZA KUTUMIA ILI KUJIINGIZIA KIPATO KUPITIA BLOG NA
       KUFIKIA MALENGO YAKO.
   DIR By: Godfrey Mtega
       Date: October 29, 2016, 8:04 am
       ---------------------------------------------------------
       KARIBU SANA MSOMAJI WA MAKALA MBALIMBALI KATIKA BLOG YETU(MTEGA
       BLOG)
       MATUMIZI YA BLOG
       1.KUWEKA HABARI NA TAARIFA MBALAMBALI.
       Unaweza kutumia blog yako kuweka au kutangaza habari mbalimbali
       za kikanda,kitaifa au hata za kimataifa.Habari kwa
       maandishi,Habari kwa Picha na Habari kwa Sauti na Habari kwa
       Video,Chaguo ni lako.
       2.KUWEKA TAARIFA ZAKO BINAFSI
       Unaweza kutumia BLOG kutunzia taarifa zako mbalambali kama vile
       matukia\o yako ya kila siku,taarifa zako za nyumbani n.k
       ANGALIZO:KAMA UNATAKA UWEKE TAARIFA ZA SIRI IWEKE BLOG YAKO
       KATIKA PRIVATE,Baada ya kufanya hivyo hakuna mtu yeyote
       atakayeweza kuona taarifa zako hata kama akaingia katika BLOG
       YAKO.
       3.Kutangaza biashara yako
       NDIO, Kama una biashara yako na unataka kuinadi kupitia blog
       basi inawezekana kabisa hapa kuna mbinu zinazohitajika ili uweze
       kufanikiwa katika hili.Lugha ya Mvuto,Utumiaji mzuri wa
       Picha,kuwa Mbunifu na jifunze jinsi ya kuongea na wateja.Toa ofa
       na mengineyo.
       4.KUTUMIA BLOG KWA AJILI YA MAWASILIANO KATIKA KAMPUNI
       Kivipi, unaweza kuitumia blog yako kwa ajili ya mawasiliano ya
       kampuni au Shirika mara nyingi blog za aina hii huwa zinwekewa
       password hivyo Mtu asiyehusika hawezi kuingia.Hata wewe unaweza
       kufanya pia.
       5.Kutumia Blog katika Taasisi Mbalimbali
       Unaweza pia Kuitumia Blog katika taasisi mbalimbali kama vile
       Shule,Vyuo,Taasisi za kidini na hata Vikundi mbalimbali.Blog
       itasaidia kurahisisha Mawasiliano.Kwa mfano Blog ya Shule
       inaweza KUTUMIKA kuweka taarifa mbalimbali na matukio ya
       Shule/Chuo kama vile Ratiba ya Vikao,Ratiba za Mitihani na
       mengineyo.Blog ya shule na Chuo pia inaweza kutumika kuweka
       JOINING INSTRUCTIONS(Hii ni barua inayotoa mwongozo wa MAELEKEZO
       Y KUJIUNGA NA CHUO AU SHULE HUSIKA) Kumekuwa na ugumu wa
       kupatikana kwa barua hizi na hivyo kuwafanya wanafunzi MUDA
       MWINGINE, kusafiri umbali mrefu kwenda shuleChuo kuchukua
       JOINING INSTRUCTIONS LETTER,BLOG INAMALIZA TATIZO HILI.
       TUNAKUTENGENEZEA BLOG KWA GHARAMA NAFUU KUANZIA TZS 10,000/= TU.
       TUPIGIE 0758297744.
       ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUJIINGIZIA KIPATO
       KWA KUPITIA BLOG.
       Hii ni sehemu muhimu ambayo karibu kila anayefungua blog anataka
       afahamu jinsi gani anaweza kuingiza kipato kwa kupitia
       blog.Swali linakuja je ni kweli mtu unaweza ukaingiza fedha kwa
       kupitia blog? Jibu ni NDIO unaweza kuingiza kipato kwa kupitia
       blog.Kabla ya yote unatakiwa ufahamu kuwa fedha ni thamani na
       thamani yoyote haipatikani pasipo kuifanyia kazi,hivyo kuingiza
       fedha kupitia blog vivo hivyo inahitaji ujitoe kwa kweli.Fahamu
       pia kuwa inahitaji muda hadi uweze kuingiza kipato kupitia
       blog.Urefu wa muda unatofautiana kuna ambao wanaanza kjiingizia
       kipato ndani ya siku kadhaa wengine miezi kadhaa na wengine
       inafikia hadi mwaka au zaidi.Yote haya hutegemea Aina ya BLOG na
       makala zinazowekwa,Kwa mfano ni vigumu kuingiza fedha haraka
       kama utafungua blog ya ktoa taarifa na habari.Hata hivyo ukiwa
       Mbunifu zaidi hakutakuwa na kikwazo.
       1.KUWEKA MATANGAZO YA WATU KISHA WAKAKULIPA
       Hii ni njia namba moja na maarufu sana utakayoweza kuitumia
       kujiingizia kipato kupitia blog yako.Fahamu kuwa kuna
       wafanyabiashara ambao wanatafuta wateja mtandaoni.Ili uweze
       kumshawishi mtu aweke tangazo lake katika blog yako lazima blog
       yako iwe na vitu vifuatavyo:
       i)Lazima blog yako iwe na watembeleaji wengi.
       i)Lazima blog yako iwe hai(hii ina maana ya kwamba blog yako iwe
       inawekwa makala mara kwa mara,isiwe umeweka makala leo,kisha
       unakaa mwezi mzima haujaweka makala).
       2.Kuifanya blog yako iwe ya kulipia
       Hii ni njia ya pili unayoweza kuitumia kujiingizia kipato
       kupitia.Faida kubwa iliyopo ni kwamba wewe ndiye unaamua nani
       atazame blog yako.Unaweza ukaifunga blog yako na ikawa hakuna
       mtu anayeweza kuingia katika blog yako bila ya wewe kumruhusu.Na
       utamruhusu pale atakapofanya malipo.
       KUMBUKA:Ili kuweza kutumia njia hii na uweze kufanikiwa katika
       kujiingizia kipato kupitia blog yako ni lazima uandike vitu vya
       thamani,yaani uandike vitu ambavyo vina faida kwa watu,pia viwe
       vitu ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote bure.Usihofu
       sio kazi kubwa unachotakiwa kufanya ni kujifunza sifa au stadi
       za blogger aliyebobea.
       Blogger=Mtu anayemiliki blog au anayeandika makala katika blog
       au mwendeshaji wa blog.
       Jifunze jinsi ya kuwa Blogger aliyebobea(Mtaalamu).
       Zifuatazo ni sifa za Blogger aliyebobea(Unatakiwa uwe nazo sifa
       hizi ili uweze kujiingizia kipato kupitia Blog).Usijali sio
       lazima zote,Anza na chache Nyingine Utajifunza Baadae.
       i/.Uwezo wa kuandika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.
       ii/.Uwezo wa kufanya tafiti,Blogger anatakiwa awe na uwezo wa
       kufanya utafiti juu ya yale anayotaka kuandika.
       iii/.Blogger anatakiwa awe na uzoefu na Mitandao tafutaji(Search
       Engines) .
       .Blogger anatakiwa awe na ujuzi wa kuandika kiufasaha.Andika
       kitu kinachoeleweka.
       iv/.Kuwa na Nidhamu katika Blog yako.Weka Makala lkatika blog
       yako kwa Utaratibu Maalumu.
       v/.Ujuzi katika matumizi sahihi ya picha namichoro.Picha na
       michoro ina umuhimu Mkubwa katika ka kuonngeza mvuto wa Makala.
       .
       3.Kuweka matangazo ya Google ADsense/Adword.
       Unaweza kuweka Matangazo kutoka Google /Wordpress na Ukalipwa
       kutokana na idadi ya watembeleaji wa blog yako watakaotembelea
       Blog hiyo.Kuna sifa za kuweza kuruhusiwa kuweka Matangazo ya
       Google au WordPress.
       Hii pia inahitaji blog yako iwe na makala za kutosha na iwe na
       watembeleaji wakutosha.
       4.Kutoa kozi mbalimbali ambazo watu watakuwa tayari kujiunga
       nakozi hizo NA KUZISOMA KWA MALIPO UTAKAYOWATOZA.Hii wala si
       kazi kubwa ingawa inahitaji muda na kujitoa.Kama una ujuzi
       wowote na unataka kuwafikishia watu kisha wakulipe basi fahamu
       kuwa kupitia blog unaweza kuwafikia watu wengi sana
       utaifanikisha kazi hii kupitia blog yako.Nakushauri kutumia
       Kiswahili kwani ndiyo lugha ambayo watanzania wengi wana umahiri
       nayo kuliko lugha nyingine.
       Ili uweze kufanikisha hili unatakiwa uweke ulinzi(wa password)
       KATIKA KOZI ZAKO.
       5.Kutangaza biashara zako.
       Tukiacha kutangaza biashara za watu pia wewe mwenyewe unaweza
       kutangaza biashara zako na ukaongeza wateja kupitia blog
       yako.Hii inajumuisha bidhaa zote za mtandaoni na zisizo za
       mtandaoni.Unaweza kuandika vitabu mbalimbali kuanzia vya masomo
       hadi vya hadithi na kadhalika.Vitabu hivi utaviandika kupitia MS
       Word au program nyingine inayoweza kufanya huduma hiyo na
       utawauzia wateja kwa kuwatumia katika email zao.
       Ili uweze kupata soko la uaminifu unaweza ukaandika kitabu cha
       kwanza na kukitoa BURE KABISA au kwa Ofa.Usishangae, kufanya
       hivi kutajenga uaminifu mkubwa na kama kitabu chako kitakuwa
       kizuri basi unaweza kupata soko kubwa kwa vitabu utakavyovitunga
       baadae na kuviuza.
       KUONGEZA WATEMBELEAJI KATIKA BLOG YAKO
       1.Itangaze Blog yako katika Mitandao ya kijamii,kama vile
       Facebook,Twitter,Instagram,WhatsApp na kadhalika.
       2.Andika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.Hii itawafanya
       watembeleaji wawe wanatembelea mara kwa mara.
       3.Itangaze blog yako kwenye mitandao mikubwa yenye watembeleaji
       wengi.
       4.Kuwa na utaratibu wa kukomment katika mitandao mikubwa yenye
       watembeleaji wengi.kisha acha link ya blog yako,kwa njia hii
       unaweza kupata watembeleaji,ila jitahidi kukomment kitu chenye
       maana/thamani.
       5.Chukua maoni ya wasomaji wako na uyafanyie kazi,hii itawafanya
       wasomaji wako waendelee kutembelea blog yako kwani watakuwa
       wanakipata wanachokitaka.Ukienda kinyume na wasomaji wako
       ,wanaweza kukukimbia na kutafuta blog nyingine itakayowafaa.
       6.Weka makala katika blog yako kwa utaratibu maalumu.
       7.Andika makala za muda mrefu.Makala za muda mrefu zina manufaa
       makubwa kwani hatakama makala uliiandika mwaka uliopita bado
       itakuwa na thamani.Na watu wataendelea kuisoma kwani bado ujumbe
       unatumika.Makala za habari zinadumu kwa muda mfupi sana.
       8.Kuwa mbunifu ifanye blog yako iwe ya kuvutia,Buni Mwonekano wa
       blog yako uwe wa kuvutia,kuna rangi nyingine Ukiweka unafukuza
       watembeleaji(Color Psychology).
       9.Kichwa cha makala kinachovutia.
       Jitahidi kuandika kighwa cha makala kinachovutia ili umshawishi
       MSOMAJI Kuendelea kusoma.
       10.Watambue wasomaji wa Blog yako.
       Ni vema uwe na wasomaji 10 wa blog yako unaowatambua,kuliko kuwa
       na wasomaji 100 usiowatambua.
       Ninapozungumzia kufanikiwa kupitia BLOG yako wengi wanweza
       wakapeleka mawazo yao katika UCHUMI,HASHA sina maaan hiyo,bali
       ninachikusudia hapa ni jinsi gani unaweza kufanikiwa katika blog
       yako.Hii ni kwa sababu watu walio wengi hawadumu katika blog zao
       ,yaani mtu akifungua blog baada ya muda mfupi tu miezi kadhaa(na
       wengine hata siku kadhaa) HIVYO mtu wa aina hii ameshindwa
       kufanikiwa katika blog yake.
       Zifuatzo ni sababu zinazowafanya Watu wengi washindwe kufanikiwa
       kupitia blog zao.
       1.Kiwewe cha BLOG.
       Nini maana ya kiwewe cha blog? Kiwewe cha Blog ni hali ya mtu
       kutamani sana awe na(amiliki) blog,na kufikiria kuwa ni kazi
       rahisi sana,Ukweli ni kwamba KUTENGENEZA BLOG ni kazi rahisi
       sana,tatizo linakuja katika jinsi ya kuiendesha.Inahitaji
       nidhamu ya hali ya juu sana la sivyo safari yako ya blog
       itaishia njiani.Sababu hii huwafanya wengi waachilie mbali
       kuhusu blog na hivyo kushindwa kufikia malengo.
       2.UTIAJI Chumvi wa baadhi ya watu katika Matangazo yaao ya
       kujinadi.
       Kuna baadhi ya watu wanatia chumvi sana kiasi kwamba inaonekana
       kuwa kutengeneza/kujiingizia fedha kupitia blog ni kama kazi ya
       saa moja tu.Mfano unaweza ukakuta tangazo linalosomeka ‘’FUNGUA
       BLOG LEO UANZE KUPOKEA FEDHA’’ au “FUNGUA BLOG LEO UANZE
       KUINGIZA KIPATO CHA MAANA,SI AJABU WENGINE WANAFIKIA HATA KUSEMA
       UWE TAJIRI’’.Matangazo ya namna hii na kwa mtu mwenye uelewa wa
       chini anayachukulia kama yalivyo.Pia wanashindwa kufahamu kuwa
       hiyo ni Lugha ya kibiashara tu.SI UONGO BLOG inaweza kukufikisha
       KWENYE UTAJIRI Lakini si kwa haraka na kiurahisi namna hiyo.Watu
       wa namna hii mara nyingi huishia kufunguia blog tu na kuiacha
       kwani anakuta mambo tofauti na vile alivyoambiwa.
       3.KUKOSA CHA KUANDIKA
       Wapo wanaoshindwa kupata cha Kuandika,na hivyo huishia kati
       katika safari yao ya Blog.
       >>>SULUHISHO:Hakuna kitu kipya Duniani usiogope kuona hakuna
       kipya,utakachoandika kwa kuona kila kitu kimeshaandikwa.Andika
       tofauti na Wenzako,kuwa Mbunifu na hii ndio faida ya kufanya
       utafiti kwani utafahamu mapungufu ya wengine katika makala zao
       na utajua jinsi gani utayarekebisha kupitia makala zako mpya
       utakazoandika.
       PIA,Jijengee utaratibu wa kujisomea Soma Vitu Mbalimbali
       vitakavyokuongezea Maarifa.Soma mtandaoni,soma vitabu,soma
       magazeti n.k.Ukijijengea utaratibu wa kujisomea utaongeza
       maarifa ya kutosha yatakayokuwezesha kupata makala za
       kuandika,sio kucopy.
       4.KUTOKUWA WAVUMILIVU
       Kuifanya Blog yako iwe chanzo cha mapato inahitaji Muda wa
       kutosha.Sio rahisi kuanza kufungua Blog leo na kesho ukaanza
       kupokea fedha.Kutokana na hali hii watu wasiokuwa wavumilivu
       huamua kuachana na Blog.
       >>>SULUHISHO:Inahitaji kuwa Mvumilivu ili uweze kufanikiwa
       katika blog yako.Kuwa Mvumilivu na tumia mbinu mbalimbali
       kuiboresha blog yako.
       5.KUTOPATA WATEMBELEAJI
       Kupata Watembeleaji katika Blog yako inategemea vitu vingi.Kuna
       watu wanapofungua blog na kuona hakuna watembeleaji huamua
       kuachana na blog.
       >>>>SULUHISHO:Ili kuongeza Watembeleaji katika blog yako Tumia
       mbinu zifuatazo.
       *UNAHITAJI USHAURI KUHUSU BLOG YAKO TUANDIKIE(BURE!!)
       E-Mail:godfreymtega@gmail.com
       "TUTAKUTENGENEZEA APPLICATION YA ANDROID YA BLOG YAKO"
       TUNAKUTENGENEZEA BLOG KWA GHARAMA NAFUU KUANZIA TZS 10,000/= TU
       TUPIGIE 0758297744
       *****************************************************
       Page 1 of 1