DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ri...
*****************************************************
#Post#: 3302--------------------------------------------------
Jinsi ya kuandika habari kwenye blog ili watu waipende
DIR By: stakeholder
Date: October 20, 2016, 10:13 am
---------------------------------------------------------
Habari za majukumu. Katika uandishi wa blog kuna vitu vya
kuzingatia ili upate watembeleaji wengi kwenye blog yako na
mapato yaongezeke. Usipofuata ushauri huu itafika siku utakata
tamaa ya uandishi wa blog.
Unapoandika chochote kwenye blog hakikisha unaweka kichwa cha
habari yaani title ya habari yako. Tittle iendane na habari yako
yaani iwe summary ya story nzima. Pia tittle iwe fupi mfano
sentensi ya maneno kumi kushuka chini kama "Raisi magufuli
amtumbua mkurugenzi wa jiji la mtakuja" Uandishi huu utakusaidia
kupata watu wengi kupitia google yaani watu wanaosearch habari
kwenye mitandao.
Pili punguza kukopi habari kwenye blog nyingine na kuziweka
kwenye blog yako. Kama umeona habari hiyo itakuletea watu wengi
kwenye blog yako basi kopi ila hakikisha unaedit yaani ongeza
maneno yako na futa baadhi ya maneno kuifanya iwe tofauti na
habari uliyokopi. Ukikopi na kupaste kwenye blog unayoandika
inawezqa kupelekea blog yako kutoweka yaani kuwa deleted hapo
ujue utakuwa umepoteza ajira yako kwa sababu ya
kutojishughulisha kubuni habari zako binafsai.
Tatu hakikisha mwisho mwa habari yako unaandika jina lako kama
kama mtunzi na mwandishi mfano "Imetayarishwa na Ana tesha"
Endelea kutembelea jukwaa la chatguest kila siku ufundishwe
namna ya kutajirika kupitia uandishi wa blog
*****************************************************
Page 1 of 1