DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 3291--------------------------------------------------
Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga
DIR By: ommy
Date: October 15, 2016, 3:13 am
---------------------------------------------------------
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu
zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi
na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati
zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama
mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa
mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa
kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:
1. UGONJWA WA MOYO
Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga
yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa
mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya
kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya
mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.
Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye
ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.
2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha
madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni
kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza
kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti,
kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi
mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo
mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.
3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein,
beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika
mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A
na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’
kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu
kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.
4. KINGA YA KISUKARI
Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu
wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu
mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na
‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini
na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni
kubwa kwa watu wenye kisukari.
Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za
maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.
5. DAWA BORA YA USINGIZI
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha
homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya
viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili
moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’. Gramu 100
tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’
mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye
utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa
kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi
B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na
utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.
Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu
za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara
nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona
mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.
6. DAWA BORA YA UVIMBE
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini
sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya
vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za
maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara
yoyote mabaya hapo baadaye. Kama unasumbuliwa na uvimbe popote
jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za
maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.
7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea
isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3.
Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na
utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya
mtoto.
8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike
kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani
zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti
nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya
Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na
husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko
nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic
hyperplasia’. Wanaume kazi ni kwenu.
9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za
kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu
ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za
kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu
kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk),
zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye
ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu
kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na
kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu
kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini
unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi
zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba
zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume
zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna
mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la
kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.
10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo
linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi
wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa.
Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa
mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo
mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani
kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio
sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo
la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za
maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga
zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho
‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika
kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’.
Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na
kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa
matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa
ujumla na mambo yanayohusu njaa.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo
wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma
kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali,
huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu
mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au
kupata choo kigumu kila mara.
Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi
ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na
huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo
kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za
maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa
siku.
*****************************************************
Page 1 of 1