DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 3290--------------------------------------------------
Unajua Madhara ya Dawa za Kusimamisha Uume Kwa Muda Mrefu?
DIR By: ommy
Date: October 15, 2016, 3:11 am
---------------------------------------------------------
Kuna baashi ya wanaume wanatamani wakati wakiwa wanafanya
mapenzi na wenzi au wapenzi wao basi uume zao ziwe zinasimama
muda mrefu mathalani masaa matatu au manne au zaidi huku
wakimwaga shahawa eti tu wawaridhishe wenzi wao au ili waonekane
ni wanaume waliokamilika. Wanaume wengine wamekuwa wakitumia
dawa za kusimamisha uume kama vile viagra au dawa za asili na
zingine maarufu kama dawa za kimasai! Napenda nikwambie kwamba
hizo dawa zina madhara makubwa kwa urijali wako na uko hatarini
kuupoteza hata huo urijali mdogo uliosalia!
Kusimamisha uume kwa muda mrefu na mara nyingine kiasi cha
kufikia uume inaanza kuuma kutokana na kusimama muda mrefu
tayari ni ugonjwa. Kwa maneno rahisi ni kwamba umetumia dawa za
kuongeza nguvu ili kuua nguvu chache ulizokuwa nazo. Kitalaamu
hali hiyo ya uume kusimama muda mrefu na kuuma inaitwa
'Priapism'. Priapism hutokea pale uume inapopoteza uwezo wake wa
kuondoa damu iliyoko kwenye uume hiyo (ambayo hufanya isimame)
ili isinyae (in order to become flaccid). Hiyo hali ikidumu kwa
muda wa masaa manne husababisha seli za damu iliyoko kwenye uume
kukosa hewa ya oksijeni, hivyo kupelekea tishu katika uume kufa.
Na kadri hali hiyo inavyoendelea hupelekea damu kwenye uume kuwa
na asidi na hivyo kukosa uwezo wa kusafiri au kutembea kwenda
sehemu zingine za mwili hususan kwenye moyo! Hapo hali inakuwa
mbaya sana!
Kuna wanaume wengine wanaji-overdose viagra au madawa ya
kienyeji ili wawe wanaume shababi kwelikweli kumbe ndio wanaua
uume zao. Ndio maana watu wanaotumia madawa hayo baada ya muda
fulani hali zao za kiume zinakuwa mbaya zaidi afadhali ya jana!
Ndio maana humu katika blog nimesisitiza sana matumizi ya
vyakula na viungo kama tiba ya tatizo la ngivu za kiume!
Siwashauri kutumia hayo madawa, otherwise, keep using them for
your own risk!
Bahati mbaya au vyovyote vile kama umesimamisha uumemasaa kadhaa
hakikisha katika kipindi cha ndani ya masaa manne tafuta tiba
haraka kwa daktari! Wengine baada ya kutumia hayo madawa na uume
kusimama kama msumari masaa mengi wao hudhani dawa ni kufanya
mapenzi masaa mengi na mwanamke ili kuondokana na hali hiyo!
Tena wengine ndo hufurahia eti 'leo mwanamke fulani nitamfaidi
kweli...'. My brother you are killing yourself'!!! Hutoweza
kumkomoa mwanamke kwa kufanya mapenzi! Matibabu ya tatizo hilo
ni kunyonya damu kwa kutumia sindano itakayochomwa kwenye mshipa
wa damu uitwayo vein kwenye uume yako! Mwisho nakushauri kula
sana vyakula vya asili kama matunda na mboga za majani. Usisahau
mazoezi ya viungo.
*****************************************************
Page 1 of 1