DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
*****************************************************
#Post#: 3256--------------------------------------------------
Matokeo ya darasa la saba 2016 fuatilia hapa
DIR By: stakeholder
Date: September 11, 2016, 3:50 am
---------------------------------------------------------
Matokeo ya darasa la saba 2016 habari zote tunapeana hapa.
Hongera ewe mtoto wa darasa la saba uliyehimu darasa la saba
mwaka 2016. Nikupe pongezi nawe mlezi wa mtoto au mzazi wa mtoto
huyu ambaye anasubiri matokeo yake sasa.
Elimu bure tumshukuru mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Dr john pombe Magufuli kwa kuipa kipaumbele sekta ya elimu
Tanzania. Ndugu mzazi/ mlezi na mwalimu wa mtoto aliyehitimu
masomo yake mwaka 2016 ninaomba mtoto huyo umuendeleze asiishie
hapo alipofika. Dunia ya sasa inahitaji watu wenye elimu angalau
ya sekondari. Vinginevyo mtoto huyu ataishi katika mazingira
magumu sana. Chukulia mfano hata sekta ya kilimo ambayo zamani
sekta hii ilikuwa inaendeshwa na watu walioshindwa kujiendeleza
kielimu yaani mtoto akifeli anachukua jembe na kuingia shambani
analima anapata mazao yake vizuri tu lakini sasa kilimo nacho
kinahitaji wasomi. Zama zimebadilika kilimo kina changamoto ya
uhitaji wa kutumia teknolojia ya kisasa ili mkulima afanikiwe.
Sasa kwa elimu ya darasa la saba utafanya kilimo gani?
Shule zimejengwa za kutosha kipindi cha Rais mstaafu jakaya
mrisho kikwete wengi walimbeza kuwa shule za kata hazina viwango
vya kutoa elimu lakini leo hii ni msaada mkubwa kwa mtanzania
kwani kila kata ina shule walimu wapo madawati yapo japo kuna
changamoto ambazo zinatatuliwa na serikali ya sasa kama
kupambana na uhaba wa madawati.
Mtoto huyu anayesubiri matokeo ya darasa la saba 2016 mwanzishie
tuition au pre-form one ili mwakani akichaguliwa kidato cha
kwanza asiwe mgeni sana wa masomo ya kidato cha kwanza. Wengi
wetu ni walezi fake mtoto akihitmu masomo yake tunamwacha
anaranda randa mitaani anashinda ana bet vijiweni na kushabikia
mipira badala ya kumfundisha mtoto stadi za kazi na kumwandaa na
ngazi ya elimu inayofuata. Badilika mzazi fake na mlezi fake
wewe.
Unajiandaaje na kumpeleka mtoto huyo kidato cha kwanza 2017?
Kwanza kabisa nakushauri tuma maombi mapema shule za binafsi
angalau mbili ili kama mtoto huyo atakosa nafasi shule za
serikali basi utampeleka kwenye shule za binafsi. Endelea
kufuatilia hapa chatgues.com kila mara ili upewe taarifa na
majina ya watoto wa darasa la saba waliofaulu mtihani huo.
chatguest.com inaweza kukupa taarifa hizo kwa email yako
jisajiri dakika mbili tu ili utumiwe matokeo ya darasa la saba
2016
#Post#: 3306--------------------------------------------------
Re: Matokeo ya darasa la saba 2016 fuatilia hapa
DIR By: stakeholder
Date: October 28, 2016, 5:42 am
---------------------------------------------------------
Tazama hapa matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2016 bofya link
hii
HTML http://necta.go.tz/matokeo/2016/psle/psle.htm
*****************************************************
Page 1 of 1