URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Makala Bora
       *****************************************************
       #Post#: 3227--------------------------------------------------
       RAIS MSTAAFU  AMJIBU MWANASIASA MKONGE KINGUNGE NGOMBARI MWIRU.
   DIR By: judge
       Date: August 25, 2016, 4:36 am
       ---------------------------------------------------------
       Hatimaye yale yaliyokuwa yanasubiriwa kwa hamu kutoka kwa
       washabiki na wasio washabiki wa mwanasiasa mkongwe nchini Mzee
       Kingunge Ngombari Mwiru yametimia jana baada ya ukimya mrefu
       baada ya uchaguzi wa mwaka jana 2015 wa kuchagua Rais,Wabuge na
       Madiwani ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kati ya Mwamvuli wa
       UKAWA ulioongozwa na  aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward
       N.Lowasa alipo hama kutoka chama tawala mwezi wa nane.
       Uchaguzi huo ulivuma kila kona ambapo Dr.John Pombe Joseph
       Magufuli alipata nafasi ya kupeperusha bendela ya chama tawala
       dhidi ya mpinzani wake Edward Lowasa na hatimaye kuibuka kidedea
       kumshinda Edward Lowasa na kuwa  Rais wa Jamhuri ya muungano wa
       Tanzania Dr.John Joseph Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano
       2015-2020.
       Mwanasiasa mkongwe aliahidi kuzungumzia utendaji wa rais wa sasa
       baada ya kutimiza siku mia moja za kuwa Ikulu na kuwa
       madarakani, baadaye alipofuatwa mwanasiasa huyo ambaye naye
       alifuata nyayo za Mh.Edward Lowasa kuzungumzia utendaji wa Rais
       alisema wakati ukifika atasema anaomba wamuache.
       Jana kaibuka na kuingilia mgogoro wa kisiasa ulipo sasa kati ya
       maandalizi ya maandamano ya UKAWA waliyoyaita UKUTA na serikali
       iliyoko madarakani,ameomba viongozi wasitaafu kuingilia swala
       hilo na kumshauri rais ili kuwanusuru watanzania ambao huenda
       wakaingia kwenye vita bila kutathimini madhara yatakayotokea.
       Pia mwanasiasa huyo amesema kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne
       hana sifa za kuingia kwenye kikao cha wastaafu kutokana na
       kuvunja katiba kwa kutompitisha Mh.Edward Lowasa katika
       kinyanganyiro cha kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya chama
       tawala CCM kwenye vikao vya kamati kuu kilichofanyika mwaka
       jana.
       Naye Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye kwa sasa amepumzika
       kwake Msoga anajibu hoja ya Mwanasiasa huyo mkongwe.
       *****************************************************
       Page 1 of 1