DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 3226--------------------------------------------------
WABONGO NAKUFICHA MIAKA.
DIR By: bahati93
Date: August 25, 2016, 2:28 am
---------------------------------------------------------
Katika baathi mambo watu wenye asili ya afrika wanayo na wazungu
hawawezi kuiga ni uwezo wetu wa kufurahia na kuishi katika
maisha pasipokuwa na wasiwasi juu ya upitaji wa mda. Hali hii
imechangiwa na mambo mengi sana ambayo yanashirikiana kuendelea
kutuhamasisha kutokujali kwa mda. Jambo moja ambalo nitaligusia
ni kutokana kukaa katika mazingira mazuri yaliyotupatia kila
aina ya chakula na matunda hali hii ilipelekea wazee wetu wa
zamani kutokujali kupanga mipango itakayo wavusha siku wiki au
mwaka na hivyo suala la mipango likawekwa kando na vinasaba za
mbongo zetu hivyo basi tunajikuta katika dunia ya sasa yenye
kujali sana mda tupo nyuma kidogo na wazungu wasituseme kwa
hili.
Kutokana na ufahamu wetu kukua juu mda kwa nyakati hizi na kuona
ukweli kuhusu mda. Mda umekuwa tishio kubwa sana kwa watu
wengi wa rangi kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha juu
yake na hivyo kushindwa kujiamini mbele ya mda kama kusema miaka
ambayo anayo. Hili suala ukitaka kujua limewakumba watu wangapi
fanya utafiti katika sikukuu nyingi za kuzaliwa watu wamekuwa
wakisema wanatimiza miaka kadhaa badala ya kusema namba kamili.
Sasa kituko kikubwa ni kwa hawa watu maarufu ambao kila mtu
anataka kujua undani kuhusu wao ndio wamekuwa wakitumia kila
linalowezekana miaka yao isijulikane kama kuna mwanadada mmoja
msanii mzuri sana amekuwa komando wa kuficha umri wake tunaishia
kusikia siku za kuzaliwa.
Ni ukweli kwamba mda unatupiga chenga sana na kosa sio letu sema
lipo ndani yetu. Kutokana utafiti unaonyesha mazoea yanajengwa
wakati angali sisi ni watoto wadogo sasa sote tunajukumu
kuhakikisha kwamba watoto wetu wanakuwa na mtizamo tofauti na
sisi na hivyo kuweza kupiga hatua kwenye hili jambo dogo lenye
umuhimu mkubwa katika kipindi hichi cha utandawazi duniani.
#Post#: 3232--------------------------------------------------
Re: WABONGO NAKUFICHA MIAKA.
DIR By: judge
Date: August 26, 2016, 5:51 am
---------------------------------------------------------
imekaa vizuri
*****************************************************
Page 1 of 1