DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 3225--------------------------------------------------
MALEZI MUHIMU KWA MTOTO MDOGO.
DIR By: bahati93
Date: August 25, 2016, 2:26 am
---------------------------------------------------------
Hakika kulea mtoto mchanga ni tabu sana. Kutokana na mtoto mdogo
kuwa uwezo mkubwa wa kutambua mazingira yanayomzunguka. Hii
inatokana na sababu milango yake ya fahamu inafanya kazi
asilimia mia vituko vyake sasa ukijigusa kidogo tu ameshasikia
na hivyo kustuka kutoka usingizini na yeye kutaka usingizi wake
na hajui ataupataje itabidi alie kwasababu ndo njia pekee
anayoijua itamfanya kupata anachohitaji kama mzazi inabidi
uhakikishe kila atakacho mtoto wako anakipata haraka uwezavyo.
Kwa kufanya hili utamwezesha mtoto wako uwezo wa kutambua
kuamini katika watu ili kutatua matatizo yake hapo mbeleni
atakapokuwa mtu mzima. So kama utakutana na mtu mkubwa ambaye
kila kitu anataka kufanya mwenyewe haamini mawazo ya mtu
mwingine na hashauriki jua ya kwamba hapo awali katika utoto
wake hakutendewa wema na walezi wake hivyo basi kumfanya kukomaa
katika kutatua matatizo yake mwenyewe.
Mtoto mdogo huwa hajui vituvingi na hivyo katika maisha yake ya
utotoni hutumia kujifunza vitu muhimu katika maisha kwa kadiri
awezavyo na kwa bahati mbaya hichi pia ni kipindi ambacho
anajifunza juu ya hisia mbalimbali katika maisha kama furaha,
huzuni hamasa na hizi hisia akishajifunza kubadilika zinachukuwa
mda mwingi sana ambalo linakuwa ni jukumu zito kujitua anapokuwa
mtu mzima kama kuwa na huzuni.
Kutokana na huku kwetu kuwa na uhaba na kutokujua siekolojia ya
mtoto vitu vingi tunavyofanya wazazi kwa manufaa ya mtoto
vinaweza vikawa vinamjenga mtoto kwa upande mmoja na upande
mwingine vinambomoa. Kama ifuatavyo mtoto mdogo bado hajaweza
kumaster vizuri control ya viungo vyake hivyo basi tegemea kama
anakula basi atamwaga chakula kama kutembea ataenda kushoto
kulia so kama wewe ni baba haikupasi kumkemea kwa kumtisha
sababu hajafanya kwa makusudi ni jinsi alivyo usitake mtoto wako
afanye vitu kama anavyofanya mtu mkubwa hivyo kukosoa kila
analofanya mtoto wako kwa kumlinganisha na wewe au mtoto
mwingine au dada yake au mdogo wake humfanya mtoto kukosa hamu
ya kuishi na kujiona yeye ni mbaya hana thamani na hapo ukubwani
usishangae kumkuta anajiuza kama kahaba au kufanya mambo mengine
ya kujidhalilisha sana yote jua kua mtu huyu haoni dhamani yake
tena.
Mahitaji mhimu kwa mtoto mdogo miaka mitatu mpaka minane ni
kupongezwa, kuonyeshwa upendo wa wazi, hivi vitu vinaonekana
kama vidogo lakini ni vya umuhimu sana apo ukubwani. Mtoto mdogo
huwa anapenda kila kitu anachofanya kuwa nurse, daktari,
mwanamziki, fundi ushonaji, na fani nyingine mbalimbali bila
kusahau kucheza sasa pale mtoto wako anapoonyesha kitu
anachokifanya huwa anafanya kwa jitihada zote ili uone wakati
mwingine unafanya mambo yako ya muhimu utakuta anakuja na kuanza
kuleta usumbufu kwa mtizamo wako lakini sio hivyo kwa mtizamo
wake yeye anataka hongera zake na endapo hatazipata basi ndio
mwanzo wake kukosa kujiamini katika mambo anayofanya hapo
mbeleni kwani atakuwa hajui juu ya kujaribu na kupongezwa mtu
unajisikiaje atakuwa anaogopa kufanya. Bahati mbaya ipo kwa wale
watoto wanaofanya juu chini kubakia number moja darasani kwao na
wazazi wao kuona ni kitu cha kawaida na hivyo basi wao kukosa
uhusiano wa karibu na wazazi wao katika mafanikio yao na
malipizi yao huwa ingawa hawajakusudia hapo ukubwani
watakapokuwa na pesa zao hawataangaika kushare pamoja na wazazi
wao kwa sababu hawajui waanzie wapi hicho kitu hakipo kabisa
katika mawazo yao sasa ukaona mtu tajiri afu ukamtukana kwa
kusema anajijali mwenyewe na kusahau wazazi wake basi hujui
aliyopitia ili kufika hapo alipo sasa.
Pia katika miaka hii chini ya nane mtoto huanza kujifunza juu ya
upendo na huwa wanauelewa mkubwa kuliko wazazi tunavyozania
mfano anaweza kuona na kutamani mdoli au gari alilonunuliwa
mwenzake na wazazi wake na yeye atakuwa anafikiria kama kweli
mnampenda na kumjali basi mtamnunulia na yeye. Anaweza kusema au
kutosema kama asiposema kwa kutumia ukubwa wetu utaweza kuona
kitu ambacho mtoto wako anakipenda na kuhakikisha unamfanikishia
endapo ataomba na kupuuziwa basi utakuwa mtu wa kwanza kumtupa
mkono wakati anataka uhitaji wako sana. Hili ndio huwa tatizo
kubwa sana kama mtoto akakosa huenda hapo baadae akawa mtu
mwenye roho mbaya sana kwa kutokujua upendo unanogaje unakuta
mtu kuwa na wenzi Zaidi ya mmoja hii ni kutokana na yeye kutaka
kupata upendo ambao hapo mwanzo hakuweza kuupata kabisa na
tambua kuwa upendo ni njia mbili nipe nikupe endapo mtoto mdogo
akakosa upendo basi huenda hata akawa hana mwenza au kuachika au
kuachwa kila wakati kwa sababu hawezi kupenda na kupendwa. mtu
anajifunza haya mambo akiwa mdogo ndo basi tena usishangae kuona
mtu mzima bado hajaowa au hana watoto chanzo ni utotoni.
Endapo ni mmoja wapo wa wahanga wa kunyimwa malezi bora utotoni
cha kufanya ni kuamini unaweza kuepuka mitego ya akili hiyo kwa
kujijengea mazoea ambayo yatajibadili kama tabia tambua mawazo
ambayo yanakuajia kukuongoza kwenye njia mbaya na pia unaweza
mwambia mwenza wako juu ya matendo yako mabaya ambayo anatakiwa
kuyajua na kushirikiana kuyatatua.
Watu ambao wamefunga ndoa walioanzisha familia na ambao wapo
kwenye mahusiano kaeni mkipanga na kujiandaa kumkaribisha mtoto
wenu kuhakisha mnampatia kila jambo ambalo ni muhimu kwake hivyo
kuja kuwa mtu mzuri hapo ukubwani mwenye mafanikio ambayo
mtakula wote na hii ndio maana kamili ya kuwekeza kwa mtoto
wako. Na kama una watoto Zaidi ya mmoja hakikisha kutokuonnyesha
upendeleo wala kuwalinganisha watoto wako kwamba yupi ni bora
kuliko wenzake. Na ndo kama unaanza na mmoja basi panga uzazi wa
mpango kuhakisha watoto wote wanapata uangalizi wa kutoshoa
wakiwa uchangani kama unaweza kulea vichanga Zaidi ya kimoja
usijali wewe fyatua tuu. Weka bajeti ya midoli na nguo kwa
watotoyo wenu.
*****************************************************
Page 1 of 1