URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Makala Bora
       *****************************************************
       #Post#: 3221--------------------------------------------------
       SAFU YA USHAIRI:MADA NI MAADILI MEMA KWA JAMII
   DIR By: musnadrubeiyyah
       Date: August 24, 2016, 5:20 am
       ---------------------------------------------------------
       1:Kalamu lianza shika,maneno kuyaandika,
       Moyoni mwangu metoka,na watu taelimika,
       Kwa janga hili hakika,mioyo yaadhibika,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       
       2:Kijanaa mejisahau,katika hii dunia,
       Meeka mbele dharau,na mengi mwajifanyia,
       Kwa wasia wangu huu,hebu kwanza zingatia,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       3:We mtoto ndo kiini,katika hii dunia,
       Usije vaa vimini,ukaja kujijutia,
       Na nyi wengine acheni,katakei kuvalia,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       4:Kuiga ya ghaibuni,si vizuri nawambia,
       Yangu keni akilini,yapate wasaidia,
       Nataka muwe makini,musije mukapotea,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       5:Ukiambiwa sikia,usitake ubishani,
       Usitake kukimbia,kitumwa huko nyumbani,
       Ukweli ninawambia,wekeni haya vichwani,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       6:Mkubwa ukimuona,sisite kusalimia,
       Hata iwe kwenye kona,wajibu wako sikia,
       Kimbilia kwenye kona,heshima kumtolea,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       7:Wazazi tuwaheshimu,tukitaka radhi zao,
       Utu kwao ndo muhimu,tuwape heshima zao,
       Mesema wetu karimu,pepo ndiyo nyayo zao,
       Maadili zingatia,takuja haribikiwa.
       8:Kuendelea nataka,maneno yamenishia,
       Sitaki kuhangaika,kila nikifikiria,
       Tena kulia nataka,ila ninajizuia,
       Kwa herini kwa herini,hapa sasa nakomea.
       MTUNZI NA
       MGHANI:👇👇👇👇👇👇👇👇👇
       ''''''''''''''''''''''''''''''''''''''""""""""""""""""""""""""""""""""
       IBRAHIM_SULTAN_ROUBBEIYYAH.
       MTONI_MTONGANI_DAR_ES_SALAAM.
       Musnadrubeiyyah10@gmail.com
       0717089505.
       0659582223
       WAKA MEMBER.
       -_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_-_
       #Post#: 3222--------------------------------------------------
       Re: SAFU YA USHAIRI:MADA NI MAADILI MEMA KWA JAMII
   DIR By: stakeholder
       Date: August 24, 2016, 11:41 am
       ---------------------------------------------------------
       Kumpigia. Kura mwandishi huyu log in kisha utaona box la kupigia
       kura
       *****************************************************
       Page 1 of 1