DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 3219--------------------------------------------------
SAFU YA USHAIRI:MADA NI AFYA
DIR By: musnadrubeiyyah
Date: August 24, 2016, 4:10 am
---------------------------------------------------------
AFYA
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
1:Kalamu ninaishika,Kueleza ya moyoni,
Sitaki kubabaika,Nikachosha zenu mboni,
Lengo haya kusomeka,Kufika kote nchini,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
2:Jambo moja lishikeni,Nataka kuwaambia,
Tena lizingatieni,Musije kuliachia,
Haya magonjwa jamani,Nchini yaloingia,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
3:Yanakuja maradufu,Hapa kwetu tanzania,
Mpaka mtu yu mfu,Shimoni anaingia,
Hata kama mtukufu,Mauti tamfikia,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilo bakia.
4:Himahima tujihimu,Magonjwa kuyaepuka,
Tena tiba ndo muhimu,Kunywa dawa na kupaka,
Tusije kujilaumu,Eti ndo yametufika,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
5:Tusafishe vyoo vyetu,Kina baba kina mama,
Pamoja na nyumba zetu,Tukitaka usalama,
Kizaa watoto wetu,Tuwafundishe kwa hima,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
6:Kwa mama wajawazito,Tusipo waangalia,
Waweza zaa watoto,Walio jidhoofia,
Wakaja pata mazito,Mpaka wakajifia,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
7:Na huko serikalini,Naomba muwe makini,
Kwa wenyeji na wageni,Wanoingia nchini
Hebu tuwakagueni,Wasije ambukizeni,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
8:Kalamu naweka chini,Simalize wino wangu,
Naomba muwe makini,Kwa huu wasia wangu,
Mazuri yachukueni,Faida si peke yangu,
Afya zetu tuzitunze,Kwani ndo kilobakia.
MTUNZI NA MGHANI.👇👇👇👇👇
IBRAHIM_SULTAN_ROUBBEIYYAH.
musnadrubeiyyah10@gmail.com
0717089505
0659582223
WAKA MEMBER
☑☑☑☑☑☑☑☑☑☑☑☑
#Post#: 3223--------------------------------------------------
Re: SAFU YA USHAIRI:MADA NI AFYA
DIR By: stakeholder
Date: August 24, 2016, 11:58 am
---------------------------------------------------------
Mpigie kura mwandishi huyu kama umeipenda makala hii
*****************************************************
Page 1 of 1