DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 2828--------------------------------------------------
ajira za walimu 2016 soma hapa habari mpya kuhusu post za walimu
2016
DIR By: mastory
Date: February 16, 2016, 3:30 am
---------------------------------------------------------
"
HTML https://3.bp.blogspot.com/-bA6bs0ucc_s/VsLSNGbc5HI/AAAAAAAABBY/a6ozrs-ZLmk/s400/Jaffo-16Feb2016.png
Serikali inatarajia kutoa ajira 40,000 kwa walimu wa shule za
msingi na sekondari mwaka huu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, alilieleza Nipashe jana
kuwa idadi hiyo inalenga kupunguza upungufu wa walimu shuleni.
Jaffo alisema ajira hizo zitatangazwa mapema mwaka huu na
zitaongeza nguvu kwenye shule zenye uhitaji wa walimu hasa mpya
na zile zilizoandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza na
kidato cha kwanza.
Sambamba na hilo, ameahidi kushirikiana na Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke kuwezesha wanafunzi zaidi ya 5,800 wa Shule
ya Msingi Majimatitu wanapata elimu bora.
Alisema idadi hiyo ya wananfunzi ni sawa na idadi ya shule sita
za msingi, hivyo itagawanywa katika shule za jirani pamoja na
kujenga madarasa mapya katika shule hiyo.
“Ongezeko hili la wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza
mwaka huu limetokana na mfumo wa serikali kutoa elimu bure na
lengo la serikali ni kutoa elimu bora, hivyo kama serikali
tutahakikisha tunaboresha mazingira kwa kuweka madawati ya
kutosha, madarasa na walimu, hivyo hakuna mwanafunzi atakayekaa
chini kuanzia mwezi wa sita,” alisema Jaffo.
Pia alisema serikali itahakikisha inaongeza majengo katika shule
hiyo pamoja na kujenga shule mpya umbali wa kilomita moja kutoka
shule hiyo ilipo, katika kiwanja kilichotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi mstaafu, Balozi Martin Lumbanga, kwa ajili ya kujenga
shule mpya.
Alimtaka Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Photidas Kagimbo,
kuangalia uwezekano wa kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja
hicho ili kukidhi mfumuko wa wanafunzi wanaoandikishwa kila
mwaka pamoja na kupunguzia wanafunzi wa Shule ya Mbagala
Majimatitu katika shule hiyo mpya.
Pia aliwataka kuwashirikisha wamiliki wa viwanda wa manispaa
hiyo, mchakato wa ujenzi wa madarasa ili kukamilisha kazi hiyo
kwa wakati.
Jafo pia alimtaka Ofisa Elimu wa wilaya hiyo, Angel Frank,
kuhakikisha walimu wa shule hiyo wanaotakiwa kupandishwa daraja
wanafanyiwa hivyo pamoja na kulipwa mishahara stahiki kwa wakati
kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya kulea watoto hao.
Naye Mkuu wa shule hiyo, Abdallah Ngomi, alisema shule ina
zaidi ya wanafunzi 5,800, walimu 77 wakati mahitaji yakiwa ni
walimu 131 na madawati 900 hali inayowalazimu kuweka madawati 52
katika darasa moja badala ya 15 huku mahitaji ya kwa shule
nzima yakiwa ni 1,959.
“Tuna uhitaji wa vyumba vya madarasa 131 na kwa sasa tunavyo 22
pekee na tunatarajia kujenga 10, hivyo mahitaji ni 109, matundu
ya vyoo pia tunahitaji 203 wakati tunayo 36 tu.
"Kutokana na idadi hiyo kubwa, wanafunzi wanalazimika kusomea
nje na wengine kuingia kwa awamu,” alisema.
Mwaka huu shule hiyo imeandikisha wanafunzi 1,022 wa darasa la
kwanza idadi ambayo ni sawa na wanafunzi wa shule moja."
chanzo nipashe
Jisajiri hapa chatguest kupitia link yangu hapo chini ili nikupe
taarifa kwenye email yako siku wakitangaza post za ualimu 2016
#Post#: 2835--------------------------------------------------
Re: ajira za walimu 2016 soma hapa habari mpya kuhusu post za
walimu 2016
DIR By: Wilson John
Date: February 16, 2016, 8:11 am
---------------------------------------------------------
Wafanye haraka katika kuajiri walimu maana hali si nzuri kwa
shule zetu waache kuwaweka pia vijana mda mrefu kitaa.
#Post#: 2949--------------------------------------------------
Re: ajira za walimu 2016 soma hapa habari mpya kuhusu post za
walimu 2016
DIR By: moses nyingi
Date: February 20, 2016, 1:06 pm
---------------------------------------------------------
lini serikali itaajili walimu maana shule zetu zimelemewa kwa
kuwa na wanafunzi wengi kupita uwezo
*****************************************************
Page 1 of 1