URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
       *****************************************************
       #Post#: 2534--------------------------------------------------
       mbinu za kufanikiwa kimaisha na kujiajiri
   DIR By: Yasini Hemed
       Date: November 23, 2015, 5:06 pm
       ---------------------------------------------------------
       UNAWEZA KUACHA KAZI NA KUJIAJIRI
       HUENDA wengi wakashtushwa na mada hii lakini ni ukweli
       usiopingika kuwa kuiajiri ni bora kuliko kuajiriwa. Kama wewe
       umeajiriwa, unaweza kuacha kazi na kujiajiri mwenyewe. Ni rahisi
       na kamwe hutajutia uamuzi wako.
       Wengine hufananisha suala la kuacha kazi na tukio la kuruka
       kwenye dirisha la ndege ukiwa na parachuti ukitegemea kama
       litafunguka ili utue salama. Kama utajiandaa vyema, utakuwa
       sawasawa na mtu ambaye ameelekezwa vizuri namna ya kutumia
       parachute na amejiandaa barabara kiakili na kihisia.
       Utafiti unaonyesha kuwa katika kila biashara zinazoanzishwa,
       asilimia 95 huanguka ndani ya miaka mitano na 5% huendelea.
       Lakini baada ya hapo asilimia 95% ya biashara ya asilimia hii
       huanguka ndani ya miaka 5 ifuatayo. Kwa nini kiwango cha
       biashara kuanguka ni kikubwa hivi? Kwa nini watu wengi huwa
       wanafilisika? Zifuatazo ni baadhi ya sababu:
       1. Mjasiriamali kukosa uzoefu wa biashara
       2. Mjasiriamali kukosa ujuzi na maarifa ya masoko
       3. Kukosa nidhamu ya pesa
       4. Kukosa mtaji
       5. Mauzo kuwa chini
       6. Kushindwa kuendana na baadhi ya wafanyakazi wake
       7. Kuchukua mkopo mwingi bila matumizi sahihi
       8. Kukosa stadi za mafanikio katika ujasiriamali
       9. Kukosa msukumo binafsi wa kufanya mambo sahihi
       10. Kujaribu kufanya biashara nyingi sana au mambo mengi ambayo
       yote yanahitaji muda na umakini (lack of focus)
       11. Kukosa ndoto na shauku ya kufanikiwa
       12. Magonjwa na afya mbovu
       13. Tabia ya kuahirisha mambo mra kwa mara
       14. Kukata tamaa kwa urahisi mambo yanapoonekana magumu
       15. Mtazamo hasi (negative mental attitude)
       16. Hali ya kutaka kitu bila kitu.
       17. Marafiki au washirika wasio sahihi katika biashara yako
       (mkeo au mumeo aweza kuwa kikwazo)
       18. Hofu na kutokuthubu
       19. Kushindwa kufikiri kwa makini na kupenda kukisia mara kwa
       mara.
       NATAKA KUACHA KAZI, NIFANYE BIASHARA GANI?
       Mara nyingi hilo ndio swali ambalo huwa ninaulizwa sana. Watu
       hunipigia simu wakisema kuwa wamenisikia kwenye vipindi vyangu
       vya ujasiriamali (huwa naendesha vipindi vya redio vya
       ujasiriamali) na hivyo huomba ushauri wa waanze vipi na wafanye
       biashara gani
       Hilo ndiyo swali la muhimu sana kwa mtu anayetaka kuwa
       mjasiriamali na linaweza kumsaidia mtu kupata majibu sahihi ya
       kitu atakachokifanya na kumletea mafanikio maishani.
       Watu wengi wakiulizwa ni biashara gani inaweza kukupatia fedha
       kwa urahisi, hujibu kwa kuangalia watu waliofanikiwa kupitia
       biashara mbalimbali na kuzitaja biashara hizo kama ndiyo zina
       faida kubwa. Ukweli ni kwamba biashara yeyote inaweza kufanikiwa
       ikiwa itapata wateja wengi wakutosha. Hivyo suala la msingi, sio
       biashara gani ya muhimu, bali ni vigezo gani vya msingi.
       KABLA HUJAACHA KAZI ZINGATIA YAFUATAYO:
       • Chunguza siri za biashara zinazofanikiwa na mifumo iliyopo
       nyuma yake. Jaribu kuziangalia biashara za Wahindi na Waarabu
       zinazofanywa. Watu wengi huwa na wazo la bidhaa ya kuuza au hata
       kutengeneza kama vile mshumaa, rangi, shampoo nk lakini mara
       nyingi huwa hawana ujuzi wa kutengeneza mfumo mzuri wa uletaji
       wa faida.
       • Pata mlezi au mshauri (Mentor) atakayekusaidia katika safari
       ya ujasiriamali. Neno mentor linamaanisha mtu ambaye amefanikiwa
       kwenye jambo fulani na ana uwezo wa kuwasaidia/kuwaelekeza watu
       wengine wafanikiwe kama yeye.
       • Fanya kazi kwenye biashara ya mtu aliyefanikiwa na ambaye
       unataka kuja kuwa kama yeye. Wakati mwingine, njia ya mkato ya
       kujifunza biashara ni kukubali kutumika chini ya mtu mwingine
       ili ujionee moja kwa moja uendeshaji wa biashara kabla hujaamua
       kuingia moja kwa moja.
       • Jenga tabia ya kuwauliza maswali ya msingi wajasiriamali
       waliofanikiwa. Kila unapopata nafasi ya kuwa na mtu tajiri, jipe
       moyo mara kwa mara halafu uliza swali hili: “Je siri ya
       mafanikio yako ni nini?”Utashangaa jinsi ambavyo watu wengi si
       wachoyo wa siri zao za mafanikio ili mradi tu uulize katika
       mazingira mazuri yenye heshima na hekima.
       5. Jijengee uwezo wa kuuza. Uwezo wa kuwashawishi watu waweze
       kununua bidhaa yako au kutumia huduma yako ndiyo uweze kusimama
       katika ujasiriamali.
       Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri ya ujasiriamali.
       *****************************************************
       Page 1 of 1