DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 2533--------------------------------------------------
Jinsi ya kuishi na mpenzi anayependa pesa.
DIR By: Wilson John
Date: November 18, 2015, 8:02 am
---------------------------------------------------------
Leo nimekuja namada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki
zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki
sana.
Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote,
kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika
mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamekuwa na
tabia ya kupenda sana fedha!
Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi
sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana
tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini
haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana.
Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi
motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia
msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: ? Mimi
nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua
kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.?
Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni
ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi
wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za
kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo
wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.
Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana
uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele
na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi
lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha
kukuacha.
Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa
na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na
kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya
kumsaidia.
Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba
ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana
kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande
zote mbili.
Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta
kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi
umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija
akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ?out?, bila kujali
kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah.
Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka?
Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi
mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika
matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni
muhimu kuzifuata. Twende tukaone.
MWELEZE UKWELI
Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa
huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa
kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara
nitakununulia hiki na kile.
Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna
wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea!
Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ?mizinga? ili afaidi.
JENGENI KUSAIDIANA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni
kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu
ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake
ana kazi yake.
Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya
mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha
zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi.
ACHA UFUJALI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji
wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza
kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!
Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha
itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri
unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako
katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.
BAKI NA HILI
Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali
kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe
ukiwa na tatizo akusaidie.
Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero.
Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza
mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.
*****************************************************
Page 1 of 1