DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Makala Bora
*****************************************************
#Post#: 2369--------------------------------------------------
Hadithi "REMINISCE SEHEMU-01"
DIR By: snow95
Date: October 22, 2015, 5:29 pm
---------------------------------------------------------
REMINISCE
SEHEMU-01
Wakati vita ya Kagera ikielekea ukingoni mnamo April 1979,
Antony Kamalamo ndio alikua anazaliwa huku baba yake mzee Madaya
Kamalamo akiwa bado hajarejea kutoka vitani. Mzee Madaya
Kamalamo aliondoka mapema nyumbani mnamo mwaka 1978 kuelekea
kwenye uwanja wa vita mkoani Kagera bila hata kujua mkewe Bi.
Martha Kamalamo kama tayari alikua na ujauzito.
Mzee Kamalamo alikuwemo kwenye brigedia ya 201 iliofanya
mashambuluzi ya kishujaa usiku wa mwezi machi tarehe 11 had 12
nakufanikiwa kuua zaid ya askari wa Libya 200 waliokua wametumwa
na Muammar Gaddafi kuja kumsaidia Idd Amin. Yalikua ni mapigano
makali sana kwani vikosi hivi vya Muammar Gaddafi vilikua na
zana nzito za kivita kama vifaru aina ya T-54 na T-55, Magari ya
kivita aina ya BTR-40 APC, BM-21 Grand, Madege ya kivita kama
MiG-21s na Tu-22 bomber.
Katika mapigano hayo tulipoteza askari wetu hodari kadhaa
akiwemo mzee Kamalamo. Mwili wake ulifikishwa kijijini kwakwe
Nansio katika kitongoji cha Bukongo wilayani Ukerewe kwa maziko
mnamo tarehe 23 Mach 1979. Ilikua ni majonzi ndani ya familia ya
mzee Kamalamo kwani familia yake ilikua inamtegemea kwa
kilakitu.
Mzee huyu aliacha wajane watatu, Bi.Martha ambae ndio mke wake
mkubwa, Bi. Nyantengo ambae alikua wa pili kuolewa, Bi.
Nyamafwimbo ambae alikua wa mwisho kuolewa na mdogo kuliko wote
na kipenzi cha mzee Kamalamo. Bi. Nyamafwimbo alipendwa sana na
mzee huyu kuliko wake zake wote.
Kwa Bi. Martha aliacha watoto wanne (Angelica, Mathew, Chloe na
Antony), Kwa Bi. Nyantengo aliacha watoto wawili (Anita na
Abigail) na kwa Bi. Nyamafwimbo hakufanikiwa kupata mtoto kwani
hakua amekaa nae muda mrefu kabla ya vita ya Kagera kuanza
***************************************************************************
Majina ya watoto wake yote hakupenda yawe ya kilugha cha kwao
bali alipendelea sana yawe ya kiingereza kwani kulikua na mzungu
wakati ule alie kua akijiita ‘’STAN’’ ambae alikua akimfundisha
kiingereza lugha ambayo aliitamani sana walau sikumoja
kuizingumza kwa ufasaha pasi na kumumunya maneno au kukunja uso.
Kutokana na Mzee Kamalamo kupenda zaidi kujifunza kiingereza na
majina ya kiingereza pia, ndipo bwana ‘’STAN’’ alipoamua
kumuandikia orodha ndefu ya majina ya kike na ya kiume kwenye
kijitabu chake cha kumbukumbu. Hivyo basi kila mwanae alipokua
akizaliwa kama ni wa kike basi alienda kukisoma hicho kijitabu
alichoandikiwa na bwana ‘’STAN’’ kwenye orodha ya majina ya kike
na kadhalika kama ni wa kiume basi alisoma kwenye orodha ya
majina ya kiume.
Bwana ‘’STAN’’ ni mzungu mwingereza kutoka Scotland moja kati ya
nchi nne zinazounda UK (UNITED KING DOM). Zingine ni Wales,
Ireland na England. Alizaliwa mnamo mwaka 1959 mjini Falkirk
Scotland ndani ya familia ya kikikristo dhehebu la Romani
Katoliki. Baba yake alikua mscotish huku mama yake akiwa na
Mchanganyiko wa Kiyahudi na Kijerumani. Alipokua na umri wa
miaka minane alianza tabia ya kutoroka nyumbani kwao na
kuandaman na wavuvi ambao huvua katika bahari ya kaskazini
(North sea) lengo ikiwa ni kuona boti zenye mashine
zinavyokimbia ndani ya maji na umaridadi wa wavuvi katika
kuogelea. Vitu hivi vilikua burudani tosha kwa ‘’STAN’’ kwani
alikua akitumia muda mrefu zaidi kukaa maeneo ya baharini kuliko
nyumbani. Mama yake ‘’STAN’’ Bi. Aviva hakuwahi kongelea vituko
vya kijana wake huyu kwa mmewe kwani mmewe alikua mkali sana kwa
watoto wake hasa pale anapo gundua kua vijana wake hawafuati
amri na sharia zake pindi anapokua kazini. Bi. Aviva alikua
akiamini katika kuwapa watoto wake uhuru katika kipindi flani
cha maisha yao ya utotoni kutamrahisishia yeye kugundua mambo
mengi kuhusu watoto wake pamoja na vipaji vyao. Tabia yake
ilimsaidia sana ‘’STAN’’ kwani mara baada ya mama yake kugundua
kua ‘’STAN’’ ni mtu wa matukio na mdadisi wa mambo akaamua
amchagulie masomo ya Fizikia na Hisabati alipokua High school
kabla hajaingia chuo kikuu cha Westminster kusomea degree ya
Architecture and Environmental design.
***********************TO BE
CONTINUED******************************
#Post#: 2370--------------------------------------------------
Re: hadithi
DIR By: snow95
Date: October 22, 2015, 6:55 pm
---------------------------------------------------------
ipo poa
*****************************************************
Page 1 of 1