DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #0000ff; font-weight: bold;">Jo...
*****************************************************
#Post#: 2347--------------------------------------------------
kwanini Baba Askofu Method Kilaini kufunga akaunti ya facebook
DIR By: Wilson John
Date: October 15, 2015, 9:23 am
---------------------------------------------------------
Ikiwa ni wiki chache tu,tangu kuanza kutumika kwa sheria ya
makosa ya kimtandao ambayo ilitiwa saini na rais na kuwa sheria
ili kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini.hali
imekuwa tofauti na ilivyotegemewa.Hii ni baada ya wahalifu wa
kimtandao kuongezeka kila kukicha.
Kati ya watu walioathirika na wahalifu wa kimtandao ni Baba
Askofu method kilaini ambaye ni askofu wa jimbo kuu katoliki la
Bukoba.
Baba Askofu Method kilaini, amepata athari hiyo baada ya kuwepo
kwa mtu ambaye amefungua akaunti feki katika mtandao wa
facebook.Akaunti hiyo feki imekuwa ikitumia jina la Kiongozi
huyu katika kanisa kwa kuomba pesa, kwa watu mbalimbali
watumiaji wa mtandao wa kijamii hasa facebook.
Baba Askofu Ameandika uamuzi wa kufuta kabisa akaunti yake ya
facebookKupitia ukurasa wake huo, na kuwaomba radhi marafiki
zake takribani elfu nne wanaomfuatilia na kuungana nae.Hali kama
hiyo imewatokea pia viongozi mbalimbali wa siasa nchini,ambapo
watu kadhaa walishitakiwa kwa utapeli na kughushi akaunti feki
za viongozi nchini.
je unadhani kuanza kutumika kwa sheria ya makosa ya kimtandao
nchini Tanzania kuna uwezekano wa kupunguza matumizi holela ya
mitandao.?
#Post#: 2349--------------------------------------------------
Re: kwanini Baba Askofu Method Kilaini kufunga akaunti ya
facebook
DIR By: udaku
Date: October 15, 2015, 10:20 am
---------------------------------------------------------
Hiyo sheria itawaogopesha wengi kutumia mitandao ya kijamii.
lakini baba askofu aje hapa chatguest kuna usalama mkubwa na ni
rahisi kumkamata tapeli anayetumia majina ya watu maarufu. Pole
baba askofu
*****************************************************
Page 1 of 1