URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Na...
       *****************************************************
       #Post#: 2268--------------------------------------------------
       Jihadhari na matapeli wanaotumia jina la kampuni ya stamigold
       biharamulo
   DIR By: mastory
       Date: September 10, 2015, 12:53 pm
       ---------------------------------------------------------
       KAMPUNI YA STAMIGOLD MGODI WA BIHARAMULO
       Kufuatia wimbi la Matapeli kutumia jina la kampuni wakidai kuwa
       wao ni wafanyakazi wa STAMIGOLD wenye uwezo wa kutoa ajira
       katika mgodi wa Biharamulo , kampuni ingependa kuchukua fursa
       hii kuutahadharisha Umma wa Watanzania kama ifuatavyo:
       1. Nafasi zote za ajira zilizopo au zinazotokea katika kampuni
       hutangazwa kupitia magazeti ya Serikali hususani Daily news.
       2. Kampuni haina utaratibu wa kufanya usaili (Interview) kwa
       njia ya simu.
       3. Maeneo rasmi ya kufanyia usaili (Interview) ni mgodini
       Biharamulo na mara chache katika ofisi zetu zilizopo katika
       jengo la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) barabara ya Umoja
       wa Mataifa jijini Dar es salaam.
       4. Kampuni haina utaratibu wa kutoza malipo yoyote kwa ajili ya
       usaili au kupata nafasi ya ajira.
       5. Kampuni haina makubaliano na mtu au wakala wa ajira yeyote
       (recruitment agent) katika zoezi la kuajiri.
       6. Anuani rasmi ya barua pepe itumikayo kupokea maombi ya nafasi
       za kazi pale zinapotangazwa ni hr.biharamulo@stamigold.co.tz
       Tunawaomba Watanzania wote kuwa macho na matapeli hawa
       wanaopigia watu simu na kujinadi kuwa wanaweza kuwapatia ajira
       katika kampuni ya STAMIGOLD.
       Imetolewa na:
       Ofisi ya Mawasiliano
       STAMIGOLD Biharamulo
       Plot. No. 417/418 UN Road
       S.L.P 78508 Dar es Salaam.
       Email: info@stamigold.co.tz Website: www.stamigold.co.tz
       *****************************************************
       Page 1 of 1