URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ri...
       *****************************************************
       #Post#: 2236--------------------------------------------------
       Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na hasara zake.
   DIR By: Trainer
       Date: August 24, 2015, 4:03 am
       ---------------------------------------------------------
       Teknolojia imekua sana nchini Tanzania hata kuwafanya watu wengi
       wafikiwe na huduma ya internet. Sasa uwepo wa teknolojia hii ya
       mawasiliano kwa njia ya intaneti ikitumika vibaya hakika hasara
       zifuatazo zitajitokeza, ukosefu wa amani nchini kwakua watu
       wanatumia mitandao ya kijamii kueneza uchochezi, chuki, ugaidi
       na madhara mengine yatokanayo na matumizi ya intaneti.
       Mmomonyoko wa maadili  kutokana na kutumia mitandao ya kijamii
       kuonyesha picha za ngono, kutazama video za ngono, wizi kwa njia
       ya mitandao, kupunguza uzalishaji mali kwakuwa watu wengi
       wanapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii kujadili mambo yasiyo
       na manufaa kwa jamii kama kukuza uchumi. Lakini ukitumia vizuri
       mitandao ya kijamii utafanikiwa kiuchumi, kielimu, pia utapata
       burudani uzitakazo na mambo mengine mengi yenye faida kubwa
       kwako.
       *****************************************************
       Page 1 of 1