URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 2230--------------------------------------------------
       Mwanaume anayegombania mtoto wa diamond na Zari soma hapa
   DIR By: udaku
       Date: August 20, 2015, 12:06 pm
       ---------------------------------------------------------
       [img]
  HTML https://encrypted-tbn2.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTi96GzG0TP06umkfTRVBFjaDkEN3PIn17eU0cX1a3WUKKSk_mP[/img]
       Sakata la yule jamaa aitwaye King Lawrence, raia wa Uganda
       mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ anayedai kuwa
       mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
       aliyempata kupitia kwa mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The
       Boss Lady’, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ siyo wa mwanamuziki
       huyo, limechukua sura mpya.
       Jamaa huyo amefunguka upya kwamba, ametenga mamilioni ya fedha
       kumpora Diamond bintiye Tiffah.
       KING LAWRENCE AMGEUKA IVAN
       Kabla ya kutenga mamilioni hayo, King Lawrence ambaye ni rafiki
       wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga aliposti kwenye
       akaunti yake ya Instagram kile kinachoonekana ni barua ya kutaka
       kufanyika vipimo vya DNA ili kubaini Tiffah ni damu ya nani huku
       barua hiyo ikimtaja King Lawrence kuwa ndiye mhusika.
       Pia kabla ya barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na kampuni ya
       wanasheria ya Uganda ya Web Advocates & Solicitors, King
       Lawrence alikaririwa akidai kwamba Tiffah ni damu ya Ivan hivyo
       kitendo cha kudai ni damu yake kimezidi kusababisha ‘drama’
       kwenye mitandao ya kijamii.
       Katika madai yake mapya, King Lawrence amebadilisha habari kuwa
       Tiffah ni damu ya Ivan kwa kuwa aliondoka kwa jamaa huyo akiwa
       tayari mjamzito na badala yake sasa yeye (King Lawrence) ndiye
       anadai ni baba wa Tiffah!
       ADAI KULALA NA ZARI
       Kwa mujibu wa King Lawrence anayedaiwa kuwa na njaa ya
       umaarufu, eti alilala na Zari mapema Januari, mwaka huu na kumpa
       ujauzito huo ambao umemleta Tiffah duniani hivyo yupo tayari
       kutumia gharama yoyote kumpora Diamond mtoto huyo.
       ATENGA MILIONI 70
       Ili kuthibitisha kile alichokisema, King Lawrence alitundika
       picha ya mkwanja mrefu unaokadiriwa kufikia Fedha ya Sauz
       takriban Randi 425,000 karibia Sh. milioni 70 za Kibongo ambazo
       ameapa kuzitumia kwa mawakili, wanasheria, mahakama na kwenye
       vipimo vya DNA kuhakikisha anammaliza Zari na kumchukua Tiffah.
       AMANI LAGUNDUA KITU TOFAUTI
       Wafuatiliaji wa sakata hilo wameliambia Amani kitu tofauti
       kwamba, kinachoonekana Ivan na King Lawrence wamepania
       kuhakikisha kuwa Zari na Diamond hawapati furaha ya kupata
       mtoto.
       MUNGU AMUEPUSHE TIFFAH
       Hata hivyo, hakuna chochote kinachoonekana kuwaumiza Diamond na
       Zari katika yote hayo yanayosemwa kwa sababu wana uhakika juu ya
       mtoto wao huku kila mtu akimuomba Mungu amuepushe mtoto huyo na
       drama za watu wasiokuwa na mshipa wa aibu.
       DIAMOND AFUNGUKA
       Akizungumza na Amani juu ya sakata hilo ndani ya chumba cha
       gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar mapema wiki hii, Diamond
       alifunguka kuwa, hao jamaa wanatafuta umaarufu na kwamba hakuna
       barua yoyote aliyopelekewa Zari.
       Diamond alisema kuwa barua ya kudai mtoto wake akapimwe DNA
       bado haijamfikia na kama ni ishu ya kisheria inayohusu mahakama
       basi ingepitia kwa wakili au mwanasheria wao na siyo kupitia
       mitandaoni.
       “Si nyumbani kwake wala ofisini kwake South wala Uganda, hakuna
       barua yoyote. Wewe umeona wapi mtu anaitwa mahakamani kwa barua
       ya kwenye ukurasa wa mtu wa social media (mitandao ya kijamii)?”
       Alihoji Diamond akionekana ‘kumaindi’ juu ya ishu hiyo na
       kuhoji: “Huyu jamaa, hivi hana kazi ya kufanya?”
       AMBANA ZARI
       Mkali huyo wa Ngoma ya Nana aliendelea kutiririka kuwa,
       alimbana Zari ambaye alimwambia hajawahi kuolewa na wao wameamua
       kuishi maisha yao na hawezi kufuatilia maisha ya mtu.
       Alipoulizwa juu ya taarifa kwamba, King Lawrence ametenga
       mamilioni ili kumpora mwanaye huyo, Diamond alisema mtu huyo
       anatafuta umaarufu na kwamba kuna wanaomsikiliza hivyo naye
       anaona ndiyo njia ya kumpa umaarufu.
       “Unajua kutafuta umaarufu nayo ni gharama hivyo naamini hiyo ni
       njia yake ya kutafuta umaarufu tu hana lolote na mimi
       nisingependa kujibizana na watu. Sisi tuna maisha yetu hatuna
       muda wa kufuatilia mambo ya watu,” alimalizia Diamond akisema
       kuwa mjadala huo ameufunga kwani ana uhakika Tiffah ni damu
       yake.
       ZARI NAYE
       Muda mfupi baada ya kumalizana na Diamond, Zari naye aliibuka
       kupitia akaunti yake kwenye Instagram ambapo alimshambulia King
       Lawrence kisha kumalizia kwa kumwita chizi.
       “Visasi hufanywa na watu wenye akili za kitoto. Huyo mtu (King
       Lawrence) ni chizi,” aliandika Zari.
       
       TUJIKUMBUSHE
       Tangu Zari ajifungue Agosti 6, mwaka huu, kumekuwa na maneno
       mengi juu ya mtoto wake huyo wa kike ambapo kabla ya King
       Lawrence kudai ni mwanaye, aliyewahi kuwa mume wa Zari naye
       alikuwa akitajwa kama baba wa mtoto huyo hivyo wanaume hao ambao
       ni marafiki kuibua utata na kuonekana hawana lolote zaidi ya
       kutafuta umaarufu.
       Pia kabla ya barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na kampuni ya
       wanasheria ya Uganda ya Web Advocates & Solicitors, King
       Lawrence alikaririwa akidai kwamba Tiffah ni damu ya Ivan hivyo
       kitendo cha kudai ni damu yake kimezidi kusababisha ‘drama’
       kwenye mitandao ya kijamii.
       Katika madai yake mapya, King Lawrence amebadilisha habari kuwa
       Tiffah ni damu ya Ivan kwa kuwa aliondoka kwa jamaa huyo akiwa
       tayari mjamzito na badala yake sasa yeye (King Lawrence) ndiye
       anadai ni baba wa Tiffah!
       ADAI KULALA NA ZARI
       Kwa mujibu wa King Lawrence anayedaiwa kuwa na njaa ya umaarufu,
       eti alilala na Zari mapema Januari, mwaka huu na kumpa ujauzito
       huo ambao umemleta Tiffah duniani hivyo yupo tayari kutumia
       gharama yoyote kumpora Diamond mtoto huyo.
       ATENGA MILIONI 70
       Ili kuthibitisha kile alichokisema, King Lawrence alitundika
       picha ya mkwanja mrefu unaokadiriwa kufikia Fedha ya Sauz
       takriban Randi 425,000 karibia Sh. milioni 70 za Kibongo ambazo
       ameapa kuzitumia kwa mawakili, wanasheria, mahakama na kwenye
       vipimo vya DNA kuhakikisha anammaliza Zari na kumchukua Tiffah.
       AMANI LAGUNDUA KITU TOFAUTI
       Wafuatiliaji wa sakata hilo wameliambia Amani kitu tofauti
       kwamba, kinachoonekana Ivan na King Lawrence wamepania
       kuhakikisha kuwa Zari na Diamond hawapati furaha ya kupata
       mtoto.
       MUNGU AMUEPUSHE TIFFAH
       Hata hivyo, hakuna chochote kinachoonekana kuwaumiza Diamond na
       Zari katika yote hayo yanayosemwa kwa sababu wana uhakika juu ya
       mtoto wao huku kila mtu akimuomba Mungu amuepushe mtoto huyo na
       drama za watu wasiokuwa na mshipa wa aibu.
       DIAMOND AFUNGUKA
       Akizungumza na Amani juu ya sakata hilo ndani ya chumba cha
       gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar mapema wiki hii, Diamond
       alifunguka kuwa, hao jamaa wanatafuta umaarufu na kwamba hakuna
       barua yoyote aliyopelekewa Zari.
       Diamond alisema kuwa barua ya kudai mtoto wake akapimwe DNA bado
       haijamfikia na kama ni ishu ya kisheria inayohusu mahakama basi
       ingepitia kwa wakili au mwanasheria wao na siyo kupitia
       mitandaoni.
       “Si nyumbani kwake wala ofisini kwake South wala Uganda, hakuna
       barua yoyote. Wewe umeona wapi mtu anaitwa mahakamani kwa barua
       ya kwenye ukurasa wa mtu wa social media (mitandao ya kijamii)?”
       Alihoji Diamond akionekana ‘kumaindi’ juu ya ishu hiyo na
       kuhoji: “Huyu jamaa, hivi hana kazi ya kufanya?”
       AMBANA ZARI
       Mkali huyo wa Ngoma ya Nana aliendelea kutiririka kuwa, alimbana
       Zari ambaye alimwambia hajawahi kuolewa na wao wameamua kuishi
       maisha yao na hawezi kufuatilia maisha ya mtu.
       Alipoulizwa juu ya taarifa kwamba, King Lawrence ametenga
       mamilioni ili kumpora mwanaye huyo, Diamond alisema mtu huyo
       anatafuta umaarufu na kwamba kuna wanaomsikiliza hivyo naye
       anaona ndiyo njia ya kumpa umaarufu.
       “Unajua kutafuta umaarufu nayo ni gharama hivyo naamini hiyo ni
       njia yake ya kutafuta umaarufu tu hana lolote na mimi
       nisingependa kujibizana na watu. Sisi tuna maisha yetu hatuna
       muda wa kufuatilia mambo ya watu,” alimalizia Diamond akisema
       kuwa mjadala huo ameufunga kwani ana uhakika Tiffah ni damu
       yake.
       ZARI NAYE
       Muda mfupi baada ya kumalizana na Diamond, Zari naye aliibuka
       kupitia akaunti yake kwenye Instagram ambapo alimshambulia King
       Lawrence kisha kumalizia kwa kumwita chizi.
       “Visasi hufanywa na watu wenye akili za kitoto. Huyo mtu (King
       Lawrence) ni chizi,” aliandika Zari.
       TUJIKUMBUSHE
       Tangu Zari ajifungue Agosti 6, mwaka huu, kumekuwa na maneno
       mengi juu ya mtoto wake huyo wa kike ambapo kabla ya King
       Lawrence kudai ni mwanaye, aliyewahi kuwa mume wa Zari naye
       alikuwa akitajwa kama baba wa mtoto huyo hivyo wanaume hao ambao
       ni marafiki kuibua utata na kuonekana hawana lolote zaidi ya
       kutafuta umaarufu.
       Chanzo cha story rahatupu
       *****************************************************
       Page 1 of 1