DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Sports and entertainments
*****************************************************
#Post#: 2100--------------------------------------------------
Unaelewa nini kuhusiana na utalii wa ndani?
DIR By: Trainer
Date: August 7, 2015, 2:49 am
---------------------------------------------------------
Ndugu msomaji na mtanzania mwenzangu leo ningependa tuongelee
suala muhimu nchini kwetu tanzania. Nchi iliyopendelewa kwa kuwa
na vivutio vingi vya kiutalii kama mbuga za wanyama, mabaki ya
kale na vivutio vingine vya kihistoria. Ukiwa kama mtanzania
mzalendo umeshawahi kuwahi kuwa mtalii ndani ya nchi yako? Wengi
mpaka tunakufa hatujawahi kumwona simba ana kwa ana. Tujenge
mazoea ya kutembelea mbuga za wanyama kama mikumi,ruaha,
tarangire,serengeti, manyara na nyinginezo. Toa maoni yako
kuhusiana na utalii wa ndani ili TANAPA na wizara ya mali asili
na utalii waweze kuboresha huduma za utalii na kuukuza utalii wa
ndani na uchumi wetu
*****************************************************
Page 1 of 1