DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 189--------------------------------------------------
WASIO TOA CHAKULA KWA WANAFUNZI KWENDA JELA'
DIR By: mastory
Date: July 21, 2014, 1:00 pm
---------------------------------------------------------
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, imetoa siku 14
kwa watendaji wa vijiji kuhakikisha shule zilizopo katika vijiji
vyao zinatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi, na
atakayeshindwa awekwe ndani kwa siku saba.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri hiyo, Chrispin Luanda katika mkutano wa hadhara
wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Kaengesa wilayani
hapa wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa sera ya Matokeo
Makubwa Sasa (BRN).
Alibainisha kuwa halmashauri imelazimika kutoa agizo hilo
kufuatia taarifa kuwa baadhi ya watendaji wa vijiji wamekuwa ni
kikwazo kikubwa, ambapo wamekuwa wakikwamisha utekelezaji miradi
ya maendeleo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa kutokana na baadhi ya watendaji wa vijiji kukaidi
utekelezaji wa miradi ya maendeleo, sasa ni wakati muafaka
kuanza kuwawajibisha wanaolegalega.
“Natoa siku kumi na nne kwa watendaji wa vijiji wote wahakikishe
kuwa kuanzia sasa wanafunzi wa shule zote za msingi wilayani
humu wanapata chakula cha mchana shuleni, yeyote atakayeshindwa
akamatwe na kuwekwa ndani kwa siku saba ili iwe fundisho si
kwake tu bali pia kwa wengine wanaoendekeza tabia hiyo,”
aliagiza.
Luanda alieleza kuwa changamoto kadhaa zinazozikabili shule za
msingi wilayani humo zinaweza kutatuliwa, lakini tatizo kubwa
ni baadhi ya viongozi wa serikali kutowajibika kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
Naye Ofisa Elimu Shule za Sekondari wilayani hapa, Emiliana
Fungo, alisema wazazi wanao wajibu wa kutatua changamoto za
shule wanazosoma watoto wao ili matokeo bora yapatikane.
Chanzo:Tanzani Daima
*****************************************************
Page 1 of 1