URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ma...
       *****************************************************
       #Post#: 1885--------------------------------------------------
       UTUNDU NA UBUNIFU HUJENGA AU HUBOA UNAPOKOSEKANA
   DIR By: The Marvel
       Date: July 2, 2015, 5:02 pm
       ---------------------------------------------------------
       WAPO wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa
       sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa
       katika uhusiano wao. Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti
       umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za
       baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya
       faragha ni moja wapo.
       Wapo wasichana au niseme wanawake ambao kimaumbile wana mvuto
       sana. Wamejaaliwa uzuri wa sura na kila kitu kiasi cha
       kutamaniwa na kila mwanaume wanayekutana naye.
       Lakini linapozungumziwa suala la mapenzi kwa mwanamke, wanaume
       wanaangalia vitu vingi, achilia mbali hilo la muonenako, pia
       wanaangalia utundu na ubunifu wa faragha. Hapo ndipo
       panapowakosesha raha baadhi ya wanawake wazuri.
       Wanakuwa ni wenye kupata bahati ya kupendwa lakini hao hao ndiyo
       wale ambao kila siku wanaachwa. Si jambo la ajabu huko mtaani
       kukutana na msichana mkali ile mbaya lakini akawa si mtu wa
       kutulia na mwanaume kwa muda mrefu, kwanini? Kwa sababu hayajui
       mapenzi.
       Ni tatizo siriasi ?.
       Msichana mzuri aliyeumbika kutoyajua majamboz ni tatizo na ndiyo
       maana anaweza kuwa mtu wa kulia kila siku.
       Anaweza kukumbana na malalamiko kutoka kwa mpenzi wake kwamba
       anachokipata ni tofauti na alivyotarajia. Hakuna kinachowauma
       walio wengi kama kusikia kutoka kwa wapenzi wao kuwa
       hawawaridhishi.
       Kwa maana hiyo ni tatizo siriasi lakini lina ufumbuzi wake.
       Hakuna aliyezaliwa na kuanza kutembea moja kwa moja, vile vile
       kuingia kwenye uhusiano ukawa hujui lolote siyo tatizo ila
       unachotakiwa kukifanya ni kujifunza.
       Zungumza na wataalam wa masuala ya mapenzi, soma vijarida na
       magazeti, naamini utapata elimu tosha ya kuweza kumfanyia mpenzi
       wako yale yatakayomfurahisha.
       Ugoigoi faragha kwa mwanamke ni chanzo cha wengi kusatiliwa,
       tena utasalitiwa zaidi kama kila siku utakuwa ni mtu yule yule,
       yaani hujifunzi chochote. Mwanamke lazima awe mbunifu kwa mpenzi
       wake, abuni mbinu za kumdatisha ili kuhakikisha haachwi
       kirahisi.
       Unapobaki kujisifia kuwa wewe ni mzuri wakati huna mashamsham
       yoyote itakuwa ni kazi bure. Matokeo yake sasa utashangaa mpenzi
       wako anakwenda kwa mwingine ambaye ukimuangalia na
       kujilinganisha na wewe, unaanza kujiuliza, hivi alichokifuata
       kwa yule ni nini ?.
       Hakuna kingine, kafuata majamboz. Ndiyo maana nikasema, uzuri
       wako kama hujui chochote faragha, ujiandae kusalitiwa kila siku
       na mwisho wake utaachwa.
       Ni majamboz tu ?.
       Sifa za mwanamke anayeweza kutulia kwenye uhusiano ukiachilia
       mbali uzuri wa sura na umbo, tabia njema nalo ni jambo la
       msingi. Kama umzuri, unayajua mambo ya chumbani ile mbaya ila
       huna tabia njema, ni tatizo. Waswahili wanasema, tabia njema ni
       silaha.
       Ushauri wangu
       Ili uyafurahie maisha yako ya kimapenzi, hakikisha unakuwa imara
       kila idara. Kwanza mpende mpenzi wako kwa maana halisi ya
       kumpenda halafu jitahidi kumpatia furaha ya kweli.
       Miongoni mwa mambo yanayoweza kumfurahisha mpenzi wako ni
       kumshibisha pale mnapopeana chakula cha usiku, ale ashibe na
       wewe ushibe, mtadumu.
       Mbinu za kumshibisha mpenzi wako, zipo nyingi jifunze na
       zifanyie kazi
       *****************************************************
       Page 1 of 1