DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 162--------------------------------------------------
MWALIMU MKUU WA SEKONDARI ILIYOONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA
KITAIFA AHAMA
DIR By: mastory
Date: July 20, 2014, 3:58 am
---------------------------------------------------------
MKUU wa Shule ya Sekondari Igowele iliyopo katika kijiji cha
Igowole, wilayani Mufindi Mkoani Iringa amelazimika kuhama
nyumba yake ili kulinusuru kundi kubwa la wanafunzi wapya wa
kike wa kidato cha tano waliopangiwa kujiunga na shule hiyo.
Igowole ambayo ni shule ya kata imeingia katika historia ya
elimu nchini baada ya mwaka huu kuongoza kitaifa kwa kushika
nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha sita.
Kati ya wanafunzi wake 30 waliomaliza elimu hiyo mwaka huu, 19
walipata daraja la kwanza (Division One), 10 daraja la Pili
(division two) na mmoja alijipatia daraja tatu (Division three).
Kuondoka kwa mkuu wa shule hiyo, Andrew Kauta katika nyumba hiyo
kutawawezesha jumla ya wanafunzi 30 kati ya 237 waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha tano hivi karibuni, kupata makazi ya
muda.
Kauta alisema hatarudi katika nyumba hiyo mpaka pale, tatizo la
mabweni katika shule hiyo litakapopatiwa ufumbuzi.
“Ili kuwanusuru wanafunzi hawa, ni bora nikaishi katika nyumba
yoyote kijijini; tunataka wanafunzi wote wa kidato cha tano na
sita katika shule yetu wakae bweni,” alisema.
Wanafunzi wengine wataunga na wenzao 30 wa kidato cha sita mwaka
huu katika bweni la muda mrefu lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi
87 katika mazingira ya kubanana.
Watakaobaki, kwa mujibu wa Mwalimu wa Taaluma, Isiaka Chodota
watatumia madarasa matatu kama mabweni yao ya muda.
Huyu mwalimu anastahili pongezi kwakweli
*****************************************************
Page 1 of 1