DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
*****************************************************
#Post#: 1683--------------------------------------------------
Mtihani wa kidato cha sita 2015 kuanza tarehe 4 na kuisha 27
mei soma hapa
DIR By: Trainer
Date: May 2, 2015, 12:13 pm
---------------------------------------------------------
Mtihani wa kumaliza kidato cha sita unaanza rasmi tarehe 4 mei
na kutarajiwa kuisha tarehe 27 mei 2015. Kulikuwa na upotoshaji
wa baadhi ya mitandao kuwa Baraza la mitihani limebadili ratiba
lakini Baraza la mitihani lilitoa ufafanuzi kwenye tovuti yake
ya baraza NECTA.
Ndugu wanafunzi wa kidato cha sita mtihani ndio huo umefika,
Yawezekana umesoma sana hata ukajiamini sana kuwa utafaulu tu
Lakini hata siku moja usipuuzie mtihani. Mtihani ni mtihani hata
kama umesoma vipi.
Wale wenzangu wanaojiamini sana na kujibu mtihani haraka haraka
ili waonekane kwamba wao ndiyo wanajua sana matokeo yake
wanafeli kizembe waache tabia hiyo. Hata kama umesoma sana
usijibu swali kwa pupa. Soma swali ulielewe vizuri ndipo ulijibu
swali hilo. Ikiwezekana kabla hujajibu swali lako lisome mara
tatu kwa kurirudia ndio uanze kulijibu.
Ukimaliza Kufanya mtihani wako usikimbilie nje ili watu wakuone
kuwa umemaliza mapema mtihani wako bali kaa kwenye chumba cha
mtihani ukitafakari ulivyojibu mtihani wako na kuangalia kama
kuna makosa madogo madogo ambayo umeyafanya bila kujua.
Kuna Mtaalamu moja anatoa mafunzo yahusuyo "Mbinu za kufaulu
mtihani hata kama hukujiandaa vizuri" Bonyeza hapa usome nawe
uongeze maarifa
HTML https://somahapa.wordpress.com/2015/05/02/mbinu-kumi-za-kufaulu-mtihani-hata-kama-hukujiandaa-vizuri-fuatilia-mafunzo-haya-kama-ni-mwanafunzi-lazima-utafaulu-tu-ili-kufuatilia-mafunzo-haya-mpaka-mwisho-tuma-neno-mtihani-kwenda-075687892/
Tunawatakia kidato cha sita 2015 mtihani mwema wa kumaliza elimu
ya sekondari.
*****************************************************
Page 1 of 1