DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: <span style="color: #123aab; font-weight: bold;">Ri...
*****************************************************
#Post#: 1678--------------------------------------------------
Umuhimu wa kuwa na blog kwa watangazaji wa redio na Television
DIR By: Trainer
Date: May 1, 2015, 3:14 pm
---------------------------------------------------------
Habari ndugu msomaji wa mtandao wa chatguest. Leo napenda
nizungumzie umuhimu wa kuandika blog kwa watangazaji wa redio na
Television. Tasnia ya habari inaendana na ukuaji wa teknolojia.
Mwandishi wa habari una fulsa kubwa zaidi kama utatumia uwepo wa
teknolojia ya habari na mawasiliano duniani. Wengi wetu tumekuwa
tukipuuzia vitu vingine tukizani maisha ndiyo haya tuliyo nayo.
Mtu ukipewa mshara wa laki nne au sita basi unaridhika wala
huwazi baada ya miak kadhaa utakuwa wapi na mshahara huo.
Hapa sikutaka kuchambua masiha yako ila nilitaka nikukumbushe tu
kuwa usiridhike na mshahara unaopata fikiri zaidi ili watoto
wako na wajukuu wako wasije kuishi maisha magumu uliyopitia
wewe. Nina maana usijiangalie wewe tu kuwa mshahara unaoupata
unatosha bali huo mshahara ugawanye kwa watoto wako na wajukuu
wako.
Turudi kwenye kitovu cha ujumbe wa leo. Kuna fulsa kwenye
uandishi wa blog, Ni kweli unaweza kuwa ulijaribu kuandika blog
kwa hata miaka miwili ukaona hakuna ulichopata ukaishiti blog
yako. ulifanya kosa kuitupilia mbali blog hiyo. Leo pengine
ungekuwa unafaidi matunda kama issa michuzi au Fransic Godwin
mzee wa matukio.
Biashara ya blog inakuwa taratibu kulingana na mbinu unazotumia
kuitangaza ila ikisha julikan blog yako na watu wakapenda habari
unazoripoti mara kwa mara basi nao watatembelea blog yako mara
kwa mara. kadiri wanavyotembelea blog yako ndivyo wewe mifuko
inavyozidi kutuna na mashavu yako yanazidi kunenepa. Kwa wenye
vitambi ndio balaa.
Kwanini tunasema blog ni muhimu kwa waandishi wa habari au
watangazaji
1. Blog inakufanya ujulikane zaidi mfano kwenye blog unayoandika
lazima utaweka picha yako mara kwa mara leo umevaa hivi kesho
umevaa vile pia utaandika mambo kadha wa kadha kutokana na
vitendo hivyo watu watakujua wewe ni nani kwa mavazi, maandishi
yako na vitendo vingine ambavyo siwezi kuvisema vyote ila ukiwa
na blog watu watakujua zaidi. kuliko ukiwa unaripoti habari bale
ofisini kwako, Tofauti ni kwamba pale kwenye blog mtu anaweza
kuwasiliana nawe personaly wakati ukiwa redioni au kwenye TV mtu
anakuwa anawasilsiana na wewe kama ofisi. Pale unaitangaza ofisi
hujitangazi wewe binafsi. Sasa tumia fulsa hii ya kujitangaza
zaidi kwa kutumia blog.
2. Utaongeza kipato. Nimeshaongelea swala la kutoridhika na
mshahara. Ukiwa na muda wa ziada hata saa moja tu kwa siku
wekeza kwenye blog. Hata kama blog hiyo haitakunufaisha wewe kwa
haraka basi itamnufaisha mwanao au mjukuu wako. Kuna mtaalamu wa
blog ataalikwa aje kuzungumzia umuhimu wa kumrithisha mwanao
blog. Haitakiwi mtu akifa basi na mtandao wake ufe hii haifai
katika maendeleo. Anza sasa kumshirikisha ndugu yako wa karibu
blog yako kama huna mtoto ambaye anaweza kuanza kuiendesha
pamoja na wewe. Sasa blog ni kama Taasisi.
Tuchukulie mfano chatguest au jamiiforums kama mitandao hii
itafika mahala inakufa kwasababu ya ubinafsi wa waanzilishi basi
wengi wataathilika kwakua wanachama humu wanawasiliana kupitia
mitandao hii watu wanatafutana kimapenzi, watu wanafanya
biashara humu kwa kutumiana ujumbe wa siri. Kwahiyo mitandao
kama hii lazima irithishwe kwa vizazi vijavyo. Na kadili mtandao
unavyozidi ishi ndivyo na mapato yanavyozidi kuzalishwa kwahiyo
unaweza kukuta wewe hukunufaika lakini wajukuu wanakuja
kunufaika na mtandao wako hata kama hukuweza kuufungulia kampuni
wao watafungua kampuni yaani blog inakuja kuwa kampuni kubwa
inayoingiza mabilioni. Unashangaa facebook ilianzisha na
mwanafunzi akiwa bwenini shuleni lakini leo facebook ni kampuni
kubwa na inaofisi kuu na ofisi shirikishi baadhi ya nchi
duniani. Akia mark zurckerbag bado facebook itaendelea kwani
sasa ni kampuni na kawaida ya kampuni data zinahifadhiwa
kwaajiri ya vizazi vijavyo.
Ukishaanza kupata watazamaji wengi angalau elfu tano tu kwa siku
basi pesa utakayoipata kutoka kwenye blog hiyo itaweza kuwa sawa
au zaidi ya mshahara unaolipwa na boss wako hapo redioni au
kwenye TV. Unajua kuweka tangazo moja kwenye blog yenye
watembeleaji si chini ya elfu tano kwa siku ni laki tatu tena
hii ni bei ya kindugu. Je kwenye blog unaweza kuweka matangazo
mangapi? Pia ukijiunga na google adsense na blog yako ikawa
inapata watemebeleaji zaid ya elfu tano blog yako itakuingizia
kila siku si chini ya dola za kimalekani 8 kwa mwezi utakuwa na
dola ngapi? Zibadili kwenye shilingi uone utakuwa na shilingi
ngapi za kitanzania? haya mshahara uanoupata hapo kazini ni
kiasi gani? Je ukianza kuapata watemebeleaji elfu kumi kwa siku
utapata fedha kiasi gani? Anza leo kuandika blog.
Hayo mapato ni kutoka kwenye matangazo tu sasa ukiwa unaadika
blog inayosimamiwa na chatguest unalipwa tena kwa kila
anayeitembelea blog yako, blog ikitembeewa mara 1000 unalipwa
shilingi za kitanzania 2000 kwa kiwango cha sasa blog ikisomwa
kwa siku mara elfu kumi utakuwa na shilingi ngapi? Yaani pesa
utakayolipwa toka chatguest inatosha kabisa kwa wewe kusema sasa
basi siku nzima mimi naitumia kuandika blog sitaki kazi nyingine
zaidi Ila kumbuka usiridhike na unachopata. Hata kama unalipwa
milioni na chatguest bado kibarua chako huko redioni kishikilie
ili upate zaidi.
3. Unajiwekea kumbukumbu ambayo vizaji vijavyo vitapata kukujua
kuwa ulikuwa mwandishi wa habari na habari ulizokuwa unaripoti
ni za mtindo huu. Ni rahisi kwa vizazi vijavyo kupata taarifa
zako mtandaoni kuliko kupata kwenye hard drives na cd
mlizorekodi hapo kituoni. Kwanza watu wanaweza wasipate kabisa
labda uwekewe siku yakumbukumbu kama hayati mwalimu nyerere la
sivyo wafanyakazi wapya wa maiaka hiyo ndio wachache watakao
pata kumbukumbu yako au nao wasipate kabisa. lakini blog itadumu
milele na hasa hasa kama utawajengea utamaduni wa kurithishana
watoto kwenda kwa wajukuu kwenda kwa vitukuu kwenda kwa nyanya
kwenda kwa vizazi vitakavyokuja. Lakini kama blog yako itatumia
free domain basi hata usipowarithisha watoto blog yako bado
itasomwa milele kwani haya makampuni tunaamini yataishi vizazi
na vizazi yanaweza kubadilishwa majina tu lakini data zitakuwepo
kwenye internet milele.
Kama somo hili limeeleweka au hata kama halijaeleweka sehemu
fulani na unataka ufafanuzi basi uwanja ni wako chuka mwisho
kabisa kwenye kibox cheupe andika mawazo yako hapo kisha bonyeza
post. Ningependa uchangie faida nyingine ambazo mtangazi wa
redio anazipata akiwa na blog kama dina marious Dijaro arungu na
wengineo. Karibu na tukutane tena kwenye mada inayofuata hapa
hapa chatguest.
Ni mimi mkufunzi wa jamii hapa chatguest Nakutakia siku njema
*****************************************************
Page 1 of 1