DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la wanafunzi Tanzania (JUWATA)
*****************************************************
#Post#: 1658--------------------------------------------------
Zaidi ya Wanafunzi 150 Wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu Dom
kufanya Mtihani
DIR By: Nadia
Date: April 27, 2015, 7:34 am
---------------------------------------------------------
hi habari kwakweli haipo poa kabisa kwa upande wangu
unashindwaje kujua kusoma na kuandika miaka yote ukiwa shuleni?
wanafunzi nasi!
"SERA ya Elimu inayokataza Walimu kutowafukuza wala kuwarudisha
darasani wanafunzi ambao hawajui Kusoma, Kuandika na Kuhesabu
(KKK), imeibua mapya mkoani Dodoma baada ya Wanafunzi zaidi ya
150 wanaosoma darasa la Saba ambao hawajui kusoma wala kuandika,
wakitarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka
huu.
Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu, umebaini kuwepo kwa idadi
kubwa ya wanafunzi ambao hawajui kusoma na kuandika ambao bado
wanaendelea kuhudhuria masomo darasani katika Halmashauri
mbalimbali za mkoa huo.
Takwimu za Idara ya elimu Msingi mkoani humo zinaonyesha kuwa
mwaka 2013, wanafunzi 1165 walifanya mtihani wa darasa la Saba
wakiwa hawajui usoma, kuandika na kuhesabu.
Aidha, Mwaka 2014, wanafunzi wapatao 312, pia waliingizwa katika
vyumba vya mitihani na kufanya mitihani hiyo licha ya Walimu wao
kufahamu moja kwa moja kuwa wanafunzi hao hawana uwezo wa katika
kusoma, kuandika na kuhesabu.
Akizungumza na FikraPevu Ofisini kwake Aprili 27, 2015, Ofisa
Elimu wa mkoa huo, Juma Kaponda, amekiri kuwepo kwa wanafunzi
ambao hawajui kusoma wala kuandika ambao wanatarajia kufanya
mtihani wa darasa la Saba ambao unatarajiwa kufanyika mwezi
Septemba mwaka huu.
“Sera haituruhusu kuwafukuza wala kuwarudisha madarasa, bali
utaratibu ni kwamba mzazi akihitaji iwe hivyo inafanyika lakini
wazazi wengi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao shuleni ingawa
pia kuna uzembe wa watumishi kutotimiza wajibu wetu” alisema na
kuongeza.
Mbali na hilo, alipoulizwa kama anayo idadi kamili ya wanafunzi
ambao hawajui kusoma na kuandika na wale wanaotarajia kufanya
mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu, alikiri kuwepo
idadi ya wanafunzi 163 ambao watafanya mtihani bila kujua kusoma
na kuandika.
“Kitaaluma hatupo vizuri sana lakini nawashukuru sana Walimu,
pamoja na changamoto zinazotukabili ikiwemo ya upungufu wa
nyumba za walimu na mlundikano wa wanafunzi, bado walimu
wanajituma ambapo kwa shule za Msingi mwaka 2012, ufaulu ulikuwa
asilimia 70, lakini kufikia sasa tuna ufaulu wa asilimia 90 na
Sekondari kutoka asilimia 37 na sasa tuna 64 na tunatarajia kuwa
na wastani wa asilimia 76” alikaririwa na FikraPevu.
Licha ya changamoto mbalimbali za kielimu zinazoukabili mkoa
huo, ikiwemo ya upungufu wa vyumba vya madarasa, uchunguzi
umebaini kuwa shule ya Msingi Chang’ombe B, iliyopo katikati ya
Manispaa ya Dodoma yenye wanafunzi 671, ina vyumba vya madarasa
vitatu pekee.
chanzo fikrapevu blog
*****************************************************
Page 1 of 1