URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       habari
  HTML https://habari.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
       *****************************************************
       #Post#: 1600--------------------------------------------------
       Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa upate
       habari
   DIR By: stakeholder
       Date: March 30, 2015, 9:36 am
       ---------------------------------------------------------
       Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo vya kazi  kwa
       waliomaliza mafunzo yao 2014/2015 na kusubiri kuajiriwa. Wewe ni
       moja wapo unafuatilia habari hii kila siku mitandaoni kujua kama
       serikali imeshatangaza majina ya walimu wapya 2015. Basi endelea
       kufuatia hapa chatguest.com siku majina hayo yakitangazwa tu na
       idara husika tutakujulisha uangalie umepangiwa wapi na kuanza
       kazi hiyo ya ualimu 2015.
       Kipengele hiki cha maandishi mekundu kimeongezwa tarehe 27 April
       2015 baada ya kuwa majina yametolewa na wizara husika
       Tazama majina hayo hapo chini kwa kudownload files hizo za
       walimu wa sayansi na walimu wa certificate. Chatguest
       inakurahisishia kupata habari mwambie na mwenzio
       Unaweza kutumiwa taarifa kwenye email yako kwa kujiunga hapa
       dakika 2 tu
  HTML http://www.chatguest.com/index.php?action=register
       Umefanikiwa kusomea ualimu na kuhitimu mafunzo yako ya ualimu
       2014/2015 na kusubiri wapi utapangiwa kituo cha kazi. Wapo
       wanaosubiri kuangalia wamepangiwa wapi na wakiona wamepangia
       kijijini eti wanawaza kutoripoti kituoni, ndugu kama haya ndiyo
       mawazo yako basi badili leo hii.
       Wote tukikataa kufanya kazi vijijini nani ataenda kuwakomboa
       hawa wanakijiji walio wengi Tanzania?
       Maisha mazuri yanapatikana popote pale kulingana na akili yako
       ya kutumia fulsa zilizopo hapo ulipo na kujituma kwa kazi yoyote
       ile ulibahatika kuipata. Mshukuru Mungu kwa wewe kupata kazi
       hiyo ya ualimu. Wapo waliokataa kazi ya ualimu miaka kumi
       iliyopita lakini mpaka leo hii wapo mtaani wanazunguka na
       bahasha kutafuta kazi na hawapati. karipoti kituoni kwako
       ulikopangia mapema ipasavyo na fanya kazi hiyo kwa moyo wote.
       Kwa wale wenye mtazamo wa kuwa  watafanya kazi miaka miwili tu
       ili wabadili fani hiyo ya ualimu na kusomea vitu vingine pia
       wamepotea. Kasomee kitu kingine kama una uhakika wa kupewa kazi
       na mtu unayemfahamu la sivyo utajuta kama utaende kusomea
       fanihiyo nyingine na kuacha kabisa kazi ya ualimu uliyokwisha
       ipata.
       Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
       Mitaa-(TAMISEMI) itatangaza ajira za Walimu kwa mwaka 2014/2015
       ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada wakati wowote kuanzia
       sasa. Endelea kufuatilia hapa upate kujua umepangwa wapi!
       Unaweza kutumiwa taarifa kwenye email yako kwa kujiunga hapa
       dakika 2 tu
  HTML http://www.chatguest.com/index.php?action=register
       Kwa mtazamo rahisi kabisa kati ya mwalimu anayefanya kazi
       kijijini na mwalimu anayefanya kazi mjini unadhani nani atakuwa
       anakaa na pesa muda mrefu kabla ya mshahara mwingine? Mjini
       matumizi  ni mengi kuliko kijijini hili huwezi kupinga ukipinga
       wewe asili yako ni ubishi tu. Kwahiyo usichague sehemu ya
       kufanya kazi enzi hizi za kikwete. Kipindi cha hayati
       J.K.nyerere ungeweza kuchagua sehemu ya kufanya kazi kwakua
       wataalamu walikuwa wachache leo hiii wasomi ni wengi ajira
       hazitoshi.
       Nende kijiji kijana ukalete maendeleo. Ukiwafundisha watoto hawa
       waliosahaulika kwa baadhi ya huduma utabarikiwa zaidi na Mungu
       wako. Isitoshe tuliowengi tumekulia vijijini au tumezaliwa
       vijijini sasa jiulize kama walimu waliokufundisha wewe ulipokuwa
       kujijini nao wasingekuja kuripoti wewe muda huu ungekuwa wapi
       kama sio kuchunga mbuzi za babu au za baba yako ailizorithishwa
       na baba yake.
       Kuwa mzalendo kwa hili ewe uliyesomea fani ya ualimu. Kuanzia
       leo kama ulikuwa unasema nimesomea ualimu basi tu nilitaka kuwa
       mwanasheria badili mtazamo wako na furahia kazi hiyo ya ualimu
       utaona manufaaa yake baada ya muda mfupi tu.
       Unaweza kuwa umeharibiwa saikolojia yako na jamii kwa kusikia
       kuwa eti walimu wanalipwa mishahara midogo. Si kweli
       ukilinganisha na maisha halisi ya kazi ya ualimu. Mbona walimu
       wanajenga nyumba nzuri wananunua magari mazuri hata kuliko afika
       yoyote mwingine wa serikalini unakotamani wewe ungekuwepo. Hata
       ukipata mshahara wa mabilioni kwa mwezi hautakutosha mwanadamu.
       Kadili unavyopata mshahara mkubwa ndivyo matumizi yako
       yanavyokuwa makubwa zaidi
       Kama umenielewa bonyeza alama ya f t g hapo chini kisha share
       makala hii kwa rafiki waliopo huko facebook, twitter na google
       plus nao waungane nasi kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii
       yetu.
       Basi napenda niishie hapa kwa walionielewa nawashukuru na kwa
       wasionielewa nawashukuru pia maana yake hata nisipowashukuru
       hawawezi kunielewa.
       Kama bado hujajiunga na mtandao huu wa chatguest ili tukutumie
       taarifa siku majina ya walimu wapya 2015 yatakapotangazwa basi
       jiunge kwa kubonyeza hapa
  HTML http://www.chatguest.com/index.php?action=register
       Utatumiwa
       taarifa kwenye email yako kukujuza kuwa idara husika
       imeshatangaza majina ya walimu wapya waliopangiwa vituo vya kazi
       2015
       #Post#: 1624--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: navanda
       Date: April 2, 2015, 10:06 am
       ---------------------------------------------------------
       Mimi naomba kuuliza tuliosemea post graduate diploma in
       education kama chuo cha tumaini Iringa Tutapangiwa vituo vya
       kazi kweli kuna post moja nilisoma humu inasema waliosomea post
       graduate ya education wanaweza wasipate ajira sijui ni kweli
       naomba nitoeni hofu
       #Post#: 1628--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: solomon
       Date: April 10, 2015, 10:37 am
       ---------------------------------------------------------
       Nasikia ajira za walimu zimesitishwa ni kwel? Inamana waliosomea
       ualimu watakuwa wanaaply kazi na kufanya interview kama  fani
       nyingine?
       #Post#: 1647--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: Hamis abdul
       Date: April 26, 2015, 8:12 am
       ---------------------------------------------------------
       kitu kama hicho hakiwezekani walimu bado wanahitajika kwasana tu
       mbona tunajionea wenyewe hali halisi ilivyo vijijini?
       #Post#: 1659--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: stakeholder
       Date: April 27, 2015, 7:53 am
       ---------------------------------------------------------
       Tayari majina ya walimu wapya waliopangiwa vituo vya kazi shule
       yametangazwa Unaweza kusoma Tangazo la ajira ya walimu 2015 hili
       toka wizara ya Tamisemi
       [center]
  HTML http://4.bp.blogspot.com/-Qb_iO1_kHvM/VT0lGKSLKkI/AAAAAAAASj8/MFfCuUQ_COI/s400/AA1.jpg[/center]
       Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa
       mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya
       Serikali za Mitaa.
       kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo:
       TANGAZO LA AJIRA MPYA ZA WALIMU KWA MWAKA 2015.->
  HTML http://www.pmoralg.go.tz/noticeboard/tangazo-1032-20150426-Ajira-Mpya-za-Walimu-Mwaka-2015/TANGAZO_LA_AJIRA_WALIMU_WAPYA_NA_MAFUNDI_SANIFU_MAABARA_2015.pdf
       1. Ajira za Walimu wa Cheti (Shule za Msingi) 2015. ->
  HTML http://www.pmoralg.go.tz/noticeboard/tangazo-1032-20150426-Ajira-Mpya-za-Walimu-Mwaka-2015/PLACEMENT_CERTIFICATE_27April15.pdf
       2. Ajira za Walimu wa Sayansi wa Shahada na Stashahada kwa Mwaka
       2015. ->
  HTML http://www.pmoralg.go.tz/noticeboard/tangazo-1032-20150426-Ajira-Mpya-za-Walimu-Mwaka-2015/PLACEMENT_SCIENCE_27April15.pdf
       3. Ajira za Walimu wa Masomo ya Sanaa na Biashara Ngazi ya
       Shahada na Stashahada.
  HTML http://mpekuaji.com/wp-content/uploads/2015/04/WALIMU_WA_SANAA_NA_BIASHARA_2.pdf
       chanzo Wizara ya Tamisemi
       Unaweza download mafaili haya hapa chini kujua majina ya walimu
       wa sayansi na wa certificate
       #Post#: 1660--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: suffi
       Date: April 27, 2015, 8:33 am
       ---------------------------------------------------------
       Kumbe waliosomea sanaa nao wamepata ajira. kulikuwa na ubishani
       hapa kuwa eti serikali imesema walimu wa sanaa wametosha
       hawataajiriwa tena.
       #Post#: 1661--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: Hamis abdul
       Date: April 27, 2015, 8:38 am
       ---------------------------------------------------------
       Waliosomea post graduate diploma in education tumaini university
       mbona majina siyaoni? Inamana hawaajiriwi moja kwa moja na
       serikali?
       #Post#: 1662--------------------------------------------------
       Re: Ajira mpya za walimu waliopangiwa vituo 2015 fuatilia hapa
       upate habari
   DIR By: Trainer
       Date: April 27, 2015, 11:42 am
       ---------------------------------------------------------
       Hongereni walimu mliopangiwa vituo vya kazi. Mkapige kazi sasa
       msiwe watu wakulaumu mishahara midogo kazi ngumu na kadharika.
       Manapopata nafasi ya mapumziko basi ujasiriamali kidogo nao
       utiliwe mkazo ili muweze kuongeza kipato. Sio lazima muuanzishe
       biashara zinazotakiwa kusimamiwa nanyi muda mwingi hata
       mkashindwa kutimiza majumu yenu ya kufundisha mliyopewa na
       serikali yenu Tukufu bali mnaweza kuanzisha biashara kubwa tu
       ambazo zinaweza kuendeshwa na watu mtakaowaajiri nyie walimu.
       Hapo mtakuwa mmechangia kuondoa Tatizo la ajira nchini mwenu.
       Karibuni msome makala zangu kila siku kwenye jukwaa la
       ujasiriamali kwenye mtandao huu wa chatguest. Ukiona makala
       imeandikwa na Trainer basi ndiyo mimi mshauri wa baishara
       niliyeajiriwa na mtandao huu wa chatguest.
       *****************************************************
       Page 1 of 1