DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
habari
HTML https://habari.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: Jukwaa la elimu Tanzania
*****************************************************
#Post#: 1558--------------------------------------------------
MATAPELI, AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA
VYUO VYA UALIMU
DIR By: Nadia
Date: March 24, 2015, 10:36 am
---------------------------------------------------------
HTML http://1.bp.blogspot.com/-kZnCNajG5-w/VREpMoJ19tI/AAAAAAAARyw/7gYhcFvHDiE/s800/AA1.jpg
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA
MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16
JIHADHARI NA MATAPELI
Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya
kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa
kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.
Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara
haihusiki nazo.
Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda
kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti,
Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa
sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha
zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
24 March 2015"
*****************************************************
Page 1 of 1