DIR Return Create A Forum - Home
---------------------------------------------------------
BongoTv
HTML https://bongotvuserforum.createaforum.com
---------------------------------------------------------
*****************************************************
DIR Return to: International Forum
*****************************************************
#Post#: 6--------------------------------------------------
Obama ajutia makosa ya Marekani nchini Libya
DIR By: admin
Date: April 11, 2016, 8:28 am
---------------------------------------------------------
Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba
serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.
Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati
wa utawala wake.
Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi
taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa
Kanali Muammar Gaddafi.
Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia
mafanikio na mapungufu ya utawala wake. Hata hivyo ametetea
hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa
NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya
kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi
huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa
kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika
mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya
kurejesha hali ya kawaida.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama
atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya
kuongoza kwa mihula miwili.
*****************************************************
Page 1 of 1