URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       BongoTv
  HTML https://bongotvuserforum.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: News & Events
       *****************************************************
       #Post#: 5--------------------------------------------------
       Watumishi hewa wamponza mkuu wa mkoa
   DIR By: admin
       Date: April 11, 2016, 8:27 am
       ---------------------------------------------------------
       Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
       mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.
       Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari
       kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
       Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa
       wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
       Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea.
       Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema
       amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na
       Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa kazini mara moja.
       Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada
       ya utathmini kufanywa mikoani.
       source: BBC
       *****************************************************
       Page 1 of 1