URI:
   DIR Return Create A Forum - Home
       ---------------------------------------------------------
       BongoTv
  HTML https://bongotvuserforum.createaforum.com
       ---------------------------------------------------------
       *****************************************************
   DIR Return to: General Discussion
       *****************************************************
       #Post#: 3--------------------------------------------------
       KAMA WEWE NI MBUNIFU, AU UNAKIPAJI ILA HUKITUMII KAMA Fursa ,
       SOMA HAPA
   DIR By: admin
       Date: April 11, 2016, 2:43 am
       ---------------------------------------------------------
       Habari,  ndugu msomaji na mfuatiliaji wa mtandao wetu,
       nimefurahishwa na nimetiwa moyo na historia ya Bill Gates ambaye
       alitumia kipaji chake kama fursa ambayo baadae ilimfanya awe
       tajiri mkubwa duniani . SOMA HISTORIA HII YA BILL GATES NAAMINI
       ITAKUPA UJASIRI ZAIDI KTK KUTUMIA KIPAJI/UBUNIFU ULIONAO KAMA
       FIRST YA KUKUWEZESHA KUFANIKIWA KIMAISHA "Bill Gates - (William
       Henry Gates III) Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mtu tajiri
       sana duniani na mwanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
       Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbinifu mkuu wa
       programu za kampuni ya ya Microsoft, kampuni ya programu yenye
       mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa
       programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye
       utumizi mwepesi. Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu
       hamsini na tano katika nchi themanini na tano.
       William Gates III H anajulikana kama Bill Gates alizaliwa tarehe
       28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na
       dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na
       utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini
       Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na
       Paul Allen, mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo
       wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi
       wao.
       Waliajiunga na kampuni ya kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia
       tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao ilikuwa ni kutafuta
       nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza
       kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu
       cha Harvard. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo
       kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya
       kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800.Kampuni hiyo
       iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya
       na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates
       na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea
       kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika
       chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika
       biashara.
       Mapumziko yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha
       kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya
       kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine
       zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu
       mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na
       baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile
       neno sindikizi.
       Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao
       Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia
       uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata
       hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye
       hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza
       kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya
       haukupata umaarufu vile.
       Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya
       ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali.
       Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko
       la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa
       bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
       Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa
       toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi
       GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni
       kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na
       makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana
       na mafanikio yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine
       ya Windows 95 ikifuatiwa na Windows 98, 2000, Millennium Edition
       na toleo la sasa Windows XP. Kila toleo jipya lilipotolea
       kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la
       hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft
       Office, michezo n.k. Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu
       tajiri duniani myenye thamani ya wastani wa dola bilioni
       arubaini na sita.
       Bill Gates pia ana maslahi katika biashara nyingine akiwa na
       nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo katika kampuni tofauti
       ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway Inc, Teledesic
       Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake kama
       Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo
       ya teknolojia na bidhaa mpya.
       Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994
       na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote
       wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya
       kiserikali.Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates
       Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu
       nukta mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha
       fursa ya masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza
       pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba kwa miradi ya
       jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane kwa
       miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka.
       Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango
       wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta."
       *****************************************************
       Page 1 of 1